Home » » WATATU WAFA KATIKA AJALI MUFINDI MKOANI IRINGA,10 WAJERUHIWA

WATATU WAFA KATIKA AJALI MUFINDI MKOANI IRINGA,10 WAJERUHIWA


Majeruhi Petrol Msisi ambaye ni konda wa Costa ya Mgumba akiwa wodini katika Hospital ya mafinga wilaya ya mufindi

Mmoja kati ya askari Trafiki wa wilaya ya Mufindi aliyetajwa kwa jina moja la David akimhoji mmoja kati ya wahusika wa Lori lililosababisha ajali huku Trafiki huyo akionekana kufanya kazi katika mazingira duni zaidi kwa kukaa porini kama alivyo naswa na kamera yetu
Hivi ndivyo Costa hii ya Mgumba yenye namba za usajili T 478 AGZ ilivyobanwa na lori
Lori lenye namba za usajili T 508 AGG Scania likiwa limeibana costa mali ya Mgumba katika mlima wa Changarawe mjini Mafinga
Kondakta msaidizi wa costa hiyo ya Mgumba Upendo Msambwa akiwa hoi wodini
Na Francis Godwin

Watu watatu wamekufa wengine 10 kujeruhiwa katika ajali mbili zilizotokea jana na juzi katika wilaya ya Mufindi mkoani  Iringa.

Katika ajali ya kwanza iliyotokea usiku wa kuamkia jana Pamela S.Mbise anayekadiliwa kuwa na miaka kati ya 30 ambaye ni mke wa mfanyakazi wa Sao Hill Mufindi na dereva  Taxi mjini Mafinga Edward Mgina pia anakadiliwa kuwa na miaka kati ya 30 na 31 wamekufa papo hapo baada ya gari aina ya RAV 4 ambayo walikuwa wakitumia kusafiriki kuacha  njia na kutumbukia katika mto Ruaha eneo la Misitu ya Sao Hill wilayani Mufindi .

Mashuhuda wa tukio hilo waliueleza mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kuwa watu hao walikuwa wakitokea mjini Mafinga kwenda Sao Hill na baada ya kufika eneo hilo gari lao lilitumbukia mtoni na kushindwa kujiokoa baada ya gari hilo kugeuka mataili juu kutokana na kina kirefu cha maji katika eneo hilo na hivyo gari hilo kuonekana  baada ya kupita masaa takribani mawili toka walipo zama katika mto huo.



0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa