Home » » WAJASIRIAMALI IRINGA WASEMA TPSF -DBG NI MKOMBOZI KWAO

WAJASIRIAMALI IRINGA WASEMA TPSF -DBG NI MKOMBOZI KWAO



Mjasiriamali Iringa akionyesha mafanikio yake ya kutengeneza bidhaa mbali mbali kwa kutumia chuma


Wajasirimali wa ushonaji walivyoweza kuboresha kazi zao na kuongeza mitaji yao kutokana na uwezeshaji wa DBG


Suti kali kama hii inashinwa na wajasiriamali wa DBG Iringa


MJasiriamali aliyenufaika na DBG Iringa


Viatu vyenye ubora wa hali ya juu vikiwa vimetengenezwa na mjasiriamali wa DBG Iringa


Wengi wanaongeza kiwango cha ufugaji kuku kupitia DBG Iringa


TPSF -DBG inavyowakomboa wajasiriamali Iringa


Ufugaji bora na wakisasa ulivyoongezeka Iringa



Wajasiriamali mkoani Iringa wamesema kuwa jitihada zinazofanywa na taasisi binafsi ya PTSF- DBG hapa nchini zimeendelea kuwakomboa kiuchumi kwa wao kuongeza kasi ya uzalishaji zaidi .

Wakizungumza mara baada ya sherehe fupi ya kukabidhiwa hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 67.4 mjasiriamali Michael Mlole alisema kuwa pamoja na awali kuanza katika hali ya kusuasua kazi hiyo ya ujasiriamali ila baada ya kupatiwa mafunzo ya DBG na kuwezesha wameendelea kukua zaidi kibiashara na hivyo kupongeza taasisi hiyo kwa kazi nzuri inayoendelea kuifanya hapa nchini.

Kwani alisema kuwa hivi sasa wajasiriamali hao ambao awali walikuwa wakiitwa ni wajasirimali wadogo kwa sasa wao wanajiona kuwa ni wafanyabiashara wakubwa kutokana na uwezeshaji unaofanyika chini ya DBG .

Usikose makala maalum ya jinsi ambavyo DBG ilivyoweza kuwawezesha wajasiriamali mkoa wa Iringa na Tanzania bara na Visiwani ,makala itakayokujia hivi karibuni katika mtandao huu
Picha na Habari na Francis Godwin

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa