Home » » Walimu shule ya Msingi Igeleke mjini Iringa wagoma kuishi katika nyumba za shule

Walimu shule ya Msingi Igeleke mjini Iringa wagoma kuishi katika nyumba za shule

:
Na Francis Godwin,Iringa

Huku baadhi ya shule walimu wakilalamika kukosa nyumba za walimu
na kulazimika kukimbia shule hizo ,hali hiyo ni tofauti katika
shule ya msingi Igeleke katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa baada
ya walimu wake kuzitelekeza nyumba mbili zilizojengwa na wananchi
kwa ajili ya walimu hao.

Mwandishi habari hizi  amebaini hali hiyo ya walimu kutelekeza
nyumba hizo ambazo hata hivyo bado mpya kabisa ukilinganisha na
nyumba nyingine ambazo walimu wamekuwa wakiishi mjini hapa na nje ya
mji .


Mmoja kati ya wananchi wa eneo hilo Bw.Evance
Kalinga amesema kuwa nyumba hizo ambazo zimejengwa kati ya mwaka
1994 zimeendelea kuwa ni nyumba za kulala panya na popo baada ya
walimu waliokuwa wakiishi katika nyumba hizo kuamua kuhama maeneo
hayo ya shule na kwenda kupanga kijijini

Kalinga alisema
kuwa sababu kubwa ya walimu kukimbia nyumba hizo ni kutokana na kuwa
jirani na pori na hivyo kuhofia usalama wao.

Japo alisema
kuwa ni vema uongozi wa Manispaa ya Iringa kufika na kuona jinsi
ambavyo kodi za wananchi zilivyochezewa katika eneo hilo kwa nyumba
hizo kuendelea kutumika kama maficho ya popo badala ya kutumia na
walimu hao.

Jitihada za kumpata mkuu wa shule hiyo ama
mwenyekiti wa kamati ya shule kwa kuwa ndio wasemaji wakuu wa shule
hiyo ziligonga mwamba baada ya kutokuwepo jirani na shule hiyo

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa