UTATA waibuka sakata la kuuwawa kwa watuhumiwa wa unyang’anyanyi kwa tumia silaha, Msimbe Selemani (25) na Hamisi Ibrahim wananchi wavamia kituo cha polisi Cha mjini Iringa kutaka ufafanuzi wa kufa Kwao na kuwa wanachotambua wao watuhumiwa hao walikamatwa na askari polisi walikuwa wazima. .
Wakati mtuhumiwa mmoja akipoteza maisha yake Jana mtuhumiwa wa pili amefariki usiku wa kuamkia Leo akiwa katika kituo cha polisi Iringa.
wananchi hao wakiongozwa na diwani wa kata ya Mvinjeni Frank Kalinga ( Chadema) walifika katika kituo hicho cha polisi kutaka kujua chanzo cha kifo cha mtuhumiwa huyo kabla ya polisi kumtimua diwani huyo na wananchi hao kwa Madai kuwa mtuhumiwa huyo ambaye kabla ya kuchukuliwa na polisi alipokea kipigo kikali kutoka kwa wananchi wenye hasira Kali.
Ndugu wa marehemu Selemani mkazi wa Isoka A, mjini Iringa, wamekataa kuuchukua mwili wake kutoka katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya mkoa wa Iringa.
Msemaji wa familia ya marehemu, Petro Mwani aliwaambia wanahabari kwamba ndugu yao alikuwa mzima na mwenye nguvu zake zote wakati akikamatwa na askari hao usiku wa kuamkia juzi
Wakati ndugu na wananchi wakidai kuwa ndugu mtuhumiwa huyo akikamatwa akiwa hai na kudai kuwa ameuwawa na askari polisi wawili ambao walifika kumchukua mtuhumiwa huyo jeshi la polisi limedai kuwa mtuhumiwa huyo kifo chake kimetokana na kipigo toka kwa wananchi wenye hasira Kali.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Evarist Mangalla alisema mtuhumiwa huyo alikufa majira ya saa saba usiku wa kuamkia April 10.
Alisema mtuhumiwa huyo alifia katika hospitali ya mkoa wa Iringa wakati akipatiwa matibabu baada ya kupata kipigo kikali kutoka kwa watu wenye hasira kali kwasababu ya makosa yake.
Hata hivyo mkanganyiko wa taarifa ya Polisi, umethibitishwa na ile iliyotolewa jana na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Iringa, Dk Deogratius Manyama inayoonesha kwamba Selemani alifikishwa na askari polisi katika hospitali hiyo jana majira saa 1.15 asubuhi.
Dk Manyama alisema Selemani aliyekuwa na majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake huku akiwa amevimba sana mdomo wake, alifariki dakika mbili tu baadaye baada ya kufikishwa hospitali hapo.
Alisema mpaka jana jioni mwili wa marehemu huyo haukufanyiwa uchunguzi wowote uliopaswa kufanywa kwa pamoja kati ya polsi na madaktari wa hospitali hiyo kabla ndugu wa marehemu hawajaruhusiwa kuuchukua mwili wao.
Akizungumza na wanahabari kwa uchungu jana, msemaji wa familia ya marehemu, alisema wamestushwa na taarifa za ndugu yao kufa wakati askari hao walimchukua kwa amani walipokwenda kumkamata nyumbani kwake mtaa wa Isoka A.
“Hatuwezi kuuchukua mwili wa ndugu yetu mpaka Polisi wametoa maelezo ya sababu za kifo chake kwasababu wanajua tunajua kwamba walimchukua akiwa salama,” alisema.
Alisema taarifa ya kifo cha ndugu yao waliipata katika kituo hicho cha Polisi asubuhi ya jana walipokwenda kumuwekea dhamana.
Hata hivyo Jeshi la Polisi limeshindwa kutaja majina ya askari hao likidai kwamba halina taarifa la askari wake za kuhusika katika tukio hilo.
“Tupeni muda tufanye uchunguzi, taarifa kamili kuhusiana na suala hili tutaitoa kesho asubuhi,” alisema Mangalla.
Wakati huo huo mtuhumiwa Hassan Ibarahim, aliyekamatwa pamoja na marehemu Selemani pia amefariki dunia akiwa mikononi mwa polisi katika kituo cha polisi cha IRINGA
Habari kwa Hisani ya Francis Godwin Iringa
0 comments:
Post a Comment