Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akimpa chakula mmoja kati ya wanawake wanaojisubiri kujifungua katika hospitali ya Milo Ludewa kabla ya kukabidhi msaada wa dawa
Mganga wa Hospitali ya Milo Dr Simion Mbulingwe (kulia) akimwonyesha mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe stoo ya dawa ambayo hata hivyo ilikuwa na panado pekee
Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe (kulia) akimkabidhi msaada wa dawa zenye thamani ya shilingi milioni 7.2 mganga mkuu wa Hospitali ya Milo Dr Simion Mbulingwe
Mbunge Filikunjombe akimfariji mtoto Jovitha Ngailo (4) baada ya kumpa msada wa vitu mbali mbali zikiwemo sabuni ,dawa za meno n.k pembeni ni mama mzazi wa mtoto huyo Vumilia Mtweve
Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akiwa amebeba chakula tayari kwa kula Pasaka na wagonjwa zaidi ya 50 waliolazwa katika Hospitali ya Milo
mbunge Filikunjombe akigawa matunda kwa wagonjwa wa Hospitali ya Milo wakati wa sikuu kuu ya pasaka kama ilivyoutaratibu wake wa kula na wagonjwa
MBUNGE wa jimbo la Ludewa mkoani Njombe Deo Filikunjombe amewanusuru wagonjwa wa Hospital ya Milo inayomilikiwa na Kanisa la Anglikana kufa kwa kukosa dawa kwa kukabidhi dawa dawa na mashuka 150 vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 7.2
Mbunge huyo alifikia uamuzi huo wa kuisaidia dawa Hospitali hiyo ya Milo baada ya kutembezwa katika stoo ya dawa ya Hospitali hiyo wakati wa Sherehe ya Pasaka na kushuhudia makopo matupu ya kuhifadhia dawa .
Mganga mkuu wa Hospitali hiyo Dr Simion Mbulingwe alimweleza mbunge huyo Filikunjombe katika kikao chake na watumishi wa Hospitali hiyo na viongozi wa serikali ya kata ya Milo kuwa pamoja na jitihada mbali mbali zinazofanywa na Kanisa la Anglikana katika kuendesha Hospitali hiyo ila bado kuna uhaba mkubwa wa dawa mbali mbali pamoja na kukosekana kwa gari la wagonjwa baada ya gari lililokuwepo mataili yake na Betrii kuchoka kupita kiasi .
Hivyo alisema kutokana na hali hiyo wagonjwa wanaofika kupata matibabu katika Hospitali hiyo wamekuwa wakikabiliwa na tatizo la dawa huku tatizo la gari nalo limeendelea kuiingiza Hospitali hiyo katika hasara kubwa baada ya kukamatwa mara kwa Mara na askari wa kikosi cha usalama barabarani na kutozwa faini kwa uchakavu wa taili .
Zaidi ingia hapa FRANCIS GODWIN MZEE WA MATUKIO DAIMA
0 comments:
Post a Comment