Na Francis Godwin Mzee wa matukio Daima
WAZIRI wa maliasili na utalii Ezekiel Maige amesema kuwa ofisi yake itawaburuza mahakamani watendaji wa ofisi yake pamoja na wawekezaji walionunua maeneo ya hifadhi ya Taifa inayosimamiwa na msitu wa Sao Hill Mufindi kwa njia za utapeli
Akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Ihomasa kata ya Kasanga wilaya ya Mufindi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo leo alisema kuwa hatua ya wananchi kuendelea kuuza ardhi kwa wageni si tabia nzuri na kuwa fedha wanazoziona sasa ni bora miaka ya mbele watakuja kujutia.
Waziri Maige pia alipinga utaratibu wa wananchi hao kutumia nguvu kwa kuvamia maeneo ya hifadhi na kulazimisha serikali kuwaonea huruma kwa kuwapa ardhi hiyo ambayo tayari wamejimegea bila kufuata taratibu.
Hivyo aliwataka wananchi hao wanapaswa kutumia njia sahihi ya kuomba ardhi badala ya kuendelea kuvamii maeneo ya hifadhi kwa kisingizio cha uhaba wa ardhi.
Alisema kuwa wananchi hao wanapaswa kutumia njia hiyo sahihi ya kupata ardhi na kuepuka pia na utapeli wa kuuza ardhi ya hifadhi kwa wageni .
"Wapo watanzania wenzetu wakiwemo madiwani na watendaji wa serikali za vijiji ambao wamekuwa wakiuza maeneo ya serikali kitapeli jambo ambalo linaweza kuleta migogoro isiyo ya Msingi"
Waziri Maige alisema kuwa kutokana na maombi ya mbunge wa jimbo la Mufindi kusini Mendrady Kigola la kutaka wananchi hao wapewe ardhi katika maeneo ya hifadhi ya Taifa bado hatakubali lilitokea majibu suala hilo jukwaani .
Kwani alisema kuwa kimsingi yeye analinda katiba ya nchi na kuwa hana ruhusa ya kutengua maamuzi ya serikali ya kugawa ardhi katika hifadhi.
Alisema yeye ni waziri wa maliasili na utalii hausiki na ugawaji ardhi na kuwa waziri mwenye dhamana na ardhi anapaswa kufikishiwa maombi hayo.
Wakati huo huo waziri Maige ametaka wananchi wenye matatizo ya ardhi kuweza kufikisha maombi yao na kuwa wale wenye matatizo ya ardhi kujulikana na kusaidiwa kupewa ardhi.
Pia alisema ofisi yake kamwe haitawafumbia macho wawekezaji ambao wameuziwa maeneo ya hifadhi kwa njia ya kitapeli na kuwa wale wote waliouziwa maeneo hayo watafikishwa mahakamani.
Kwani alisema kuwa kwa kawaida mwekezaji ni mtu ambaye anapaswa kufuata kanuni zote za uwekezaji na sio kuingia katika maeneo hayo kiholela.
Waziri Maige alisema suala hilo la utapeli limeingia hadi ofisi yake kwa watendaji wa misitu kufanya utapeli wa kuuza maeneo ya hifadhi na kuwa watendaji wa ardhi waliopo ndani ya wizara yake pia watafikishwa mahakamani kwa kufanya utapeli huo.
"Nasema kuwa katika suala hili la utapeli wa kuuza maeneo ya hifadhi za Taifa zitakuwa na huruma kwa mtu yeyote bila kujali nafasi yake ...wote watafikishwa mahakamani na kwa bahati mbaya sin a nafasi ya kutoa hukumu ila Kama ningekuwa na uwezo wa kutoa hokum basi kwa watendaji wa wizara yangu ningeshauri wafungwe Hata miaka 60 kwa kuhusika kufanya utapeli huo"
Waziri Maige aliagiza watendaji wa msitu wa Sao hili kwa kushirikiana na watu wa ardhi na wazee maarufu kupita katika eneo hilo lenye matatizo ya mipaka na kupimiwa upya .
Katika kumaliza mgogoro huo Waziri Maige alitoa muda wa miezi miwili hadi mwezi wa sita mipaka ya eneo hilo kuwa imepimwa na mud a wa wiki mbili kuanzia jana kuundwa kwa Kamati ya kufuatilia mgogoro huo.
Kwa upande wao wananchi hao walisema kuwa eneo hilo ambalo wanaloomba ni eneo ambalo halipo ndani ya hifadhi ila eneo la hifadhi wao wameliacha na kuendelea kulihifadhi.
0 comments:
Post a Comment