Diwani wa Chadema Kata ya Kihesa, Manispaa ya Iringa, Edgar Mgimwa amekihama chama hicho na kujiunga na CCM.
Mgimwa
amejiondoa katika chama hicho wakati kukiwa na ushindani mkali kati ya
Chadema na CCM katika uchaguzi mdogo wa udiwani kwenye kata mbili mkoani
Iringa unaotarajiwa kufanyika Novemba 26,2017.
Alitangaza
uamuzi huo jana Jumapili Novemba 5,2017 wakati wa mkutano wa kampeni za
CCM katika Kata ya Kitwiru. Kata nyingine inayofanya uchaguzi ni Kimala
iliyoko wilayani Kilolo.
Mgimwa
ameungana na wenzake watatu waliohama Chadema miezi kadhaa iliyopita
akiwemo Baraka Kimata anayewania tena udiwani katika Kata ya Kitwiru,
safari hii kupitia CCM.
Wengine
ni waliokuwa madiwani wa Viti Maalumu (Chadema), Leah Mleleu na Husna
Daudi ambao baada ya kujiuzulu walisema wataendelea kuwa wanachama wa
chama hicho.
Hata
hivyo, katika mkutano wa kampeni wa CCM jana walitangaza kujiunga na
chama hicho. Wanachama hao wapya walipokewa na Katibu wa Itikadi na
Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole.
Mgimwa akizungumza na Mwananchi leo
Jumatatu Novemba 6,2017 amesema miongoni mwa sababu zilizomfanya ahame
Chadema ni alichodai udikteta wa Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji
Peter Msigwa.
Amesema
kutokuwepo maelewano baina ya mbunge huyo na mmoja wa viongozi wa
wilaya ya Iringa kunasababisha kuzorota kwa maendeleo jambo ambalo
haliungi mkono.
Mchungaji Msigwa amesema chama hicho kina uhakika kuwa huo ni mwendelezo wa kile alichodai baadhi ya madiwani kununuliwa.
Amesema wanachokifanya sasa ni kujipanga kwenye uchaguzi mdogo ili kurejesha kata zilizokuwa zinashikiliwa na Chadema.
“Ukiwa
vitani, inapotokea askari anaanguka huna haja ya kugeuka nyuma kwa
sababu hafanyi jeshi zima kuyumba, sisi tunasonga mbele; na kwa sababu
tunajua ni mpango wa kutengeneza hatuna wasiwasi katika hilo,” amesema
Mchungaji Msigwa.
Amesema kwa sababu kata zinazoachwa wazi zitaitishwa uchaguzi mdogo, kazi yao itakuwa kuhakikisha wanashinda kwa kishindo.
Kuhusu
hilo, Katibu wa Itikadi, Hamasa na Uenezi wa CCM Manispaa ya Iringa,
Edol Bashiri ameieleza Mwananchi kuwa wataendelea kuwapokea madiwani
wengine wanaohamia chama hicho kwa kuwa milango ipo wazi.
“Wanafuata
sera safi na demokrasia inayoendeshwa kwa vitendo, tunaendelea
kuwakaribisha wengine wanaotaka kuja na tutaendelea kuwapokea,” amesema.
Bashiri amesema wanaendelea kufanya kampeni na kwamba, wapo wanachama wengine wanaohamia CCM wakitokea Chadema.
Chanzo: Mwananchi
0 comments:
Post a Comment