Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi amekabidhi mifuko ya saruji kwa ajili ya kuchochea maendeleo na kama unavyo muona akiwa anashusha safuji hiyo kutoka kwenye gari
Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi amekabidhi mifuko ya saruji akiteta jambo na wananchi waliofika katika eneo hilo alipokuwa akikabidhi saruji hizo.
Na Fredy Mgunda,Iringa
Mbunge
wa Mafinga Mjini Cosato Chumi amekabidhi mifuko ya saruji 130 kwa
ajili ya ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi ya Maarifa, kinyanmbo na
zahanati ya Rungemba kwa lengo la kuboresha maendeleo ya wananchi wa
jimbo hilo.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi msaada huo, alisema kuwa niliomba kuwa mbunge kwa
lengo la kuwatumikia wananchi hivyo najitahidi huku na kuel kuhakikisha
natimiza azma yangu ya kuleta maendeleo kwa wananchi wa jimbo la Mafinga
Mjini.
“Nimetoa
mifuko 130 ya saruji kwa ajili ya kuhamasisha ujenzi wa madarasa katika
shule mpya ya Maarifa na zahati ya Rungemba hii ni mwamzo tu
nitaendelea kutoa saruji nyingine ili kulifanya jimbo la Mafinga Mjini
kupata maendeleo kwa kasi” alisema Chumi.
Chumi
alisema kuwa halmashauri ya Mji wa Mafinga imeshaanda mpango kabambe
ambao utakuwa msaada mkubwa kuchochoe maendeleo kwa kasi huku mji ukiwa
umeshapangiliwa jinsi gani ya kuitumia vizuri ardhi ya halmashauri hii.
“Ukiangalia
miji mingi inakuwa bila kuwa na mpango kabambe kitu kinachokuja
kusababisha migogoro ya kugombea ardhi hivyo mpango huu utakuwa
namanufaa makubwa kwa jimbo hili la Mafinga Mjini” alisema Chumi.Aidha
Chumi alisema kuwa shule zilipata saruji hiyo ni shule mpya ya Maarifa
nimekabidhiwa mifuko 50 ya saruji sawa na nyingine ya Kinyanambo lakini
pia nimetoa mifuko ya saruji 30 kwa zahanati ya Rungemba lengo ni
kuchochoe kuleta maendeleo kwa wananchi.
Chumi
amewapongeza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo katika
kata za ametoa ahadi ya kuendelea kushirikiana kwa kuchangia ujenzi wa
shule zote za jimbo la mafinga mjini.Naye mwenyekiti kata ya Changalawe
Emmanuel Kuzugali ameelezea jinsi wananchi walivyochangia kuwezesha
ujenzi wa shule ya msingi utakaoanzishwa katika kata hiyo.
Kwa
upande wake diwani viti maalumu kata ya changalawe Monica Luvanda
ameelezea mchakato ulivyokuwa hadi kupelekea kushirikiana na wananchi
kuanzisha ujenzi wa shule ili kuendelea kutoa elimu bora kwa wanafunzi
wa kata hiyo.
0 comments:
Post a Comment