Home » » MILIONI MIA MOJA NA TISINI (190,000,000) ZATUMIKA KUTIBU UGONJWA WA KIPINDUPINDU HALMASHAURI YA WILAYA YA IRINGA

MILIONI MIA MOJA NA TISINI (190,000,000) ZATUMIKA KUTIBU UGONJWA WA KIPINDUPINDU HALMASHAURI YA WILAYA YA IRINGA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.


Afisa afya wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Samwel Nkya akizungumza na viongozi wa vijiji wa tarafa ya pawaga kuhusu uboreshaji wa vyoo bora kwa lengo la kutatua tatizo la ugonjwa wa kipindupindu ambalo limekuwa likijitokeza mara kwa mara katika tarafa hiyo walianza kutoa elimu kwa viongozi wote na baadae wakahamia kwa wananchi.
Afisa afya wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Samwel Nkya akizungumza na mama moja ambaye hana choo bora na kutundikiwa bendera ilikuwa inamuonyesha kuwa hana choo bora katika kijiji cha mboliboli tarafa ya pawaga mkoani Iringa.
Afisa afya wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Samwel Nkya akisimamia zoezi la utundikaji wa bendera kwa wasio na vyoo bora.

Na Fredy Mgunda,Iringa.

Halmashauri ya wilaya ya Iringa imetumia shilingi milioni mia moja na tisini (190,000,000 ) kupambana na tatizo la milipuko ya ugonjwa wa kipindupindu katika tarafa ya pawaga na Idodi mkoani Iringa na ni miongoni mwa halmashauri 156 zinazotekeleza kampeni ya kitaifa ya usafi wa mazingira Tanzania bara.

Akizungumza wakati wa utoaji elimu ya matumizi ya vyoo bora katika tarafa ya pawaga afisa afya wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Samwel Nkya aliwataka wananchi kuanza kutumia vyoo bora ili kumaliza tatizo la milipuko ya ugonjwa wa kipindupindu ambao umekuwa ukiwakumba mara kwa mara.

“Jamani chanzo mmoja wapo cha mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu ni matumizi ya vyoo ambavyo sio bora hivyo mnatakiwa kutumia vyoo bora na kutoa elimu kwa wananchi wenu maana nyinyi ndi wenye wananchi na leo tunawapa hii elimu nyie viongozi tunaomba muifikishe elimu kwa wananchi”alisema Nkya

Nkya alisema walitoa elimu ya uboreshaji wa miundombinu ya vyoo na kunawa mikono kwa kutumia maji tiririka kwa sabuni mara ya kutoka chooni kwa ngazi ya kaya na shule za msingi na sekondari,Vyuo,taasisi za kidini,taasisi binafsi,taasisi za kiserikali kama ofisi za serikali na vituo vya afya lengo likiwa ni kutokomeza kabisa ugonjwa wa kipindupindu.



0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa