Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mbunge
wa Iringa Mjini Peter Msigwa (Chadema) amekamatwa na polisi leo
Jumapili jioni baada ya kushushwa jukwaani kwenye mkutano wa hadhara
katika Kata ya Mlandege mkoani Iringa.
Mwenyekiti
wa Baraza la Vijana wa Chadema Iringa Mjini (Bavicha), Leonce Marto
aliliambia Mwananchi kuwa mbunge huyo alikamatwa saa 11:24 jioni na Mkuu
wa Upelelezi wa Mkoa (RCO) aliyekuwa ameambatana na polisi wengine
kisha wakampeleka ofisi za mkoa za jeshi hilo.
“Kutoka
Mlandege mpaka ofisini kwa kamanda wa mkoa amebadilishwa kwenye magari
matatu. Tunahisi atakuwa anasafirishwa ingawa bado anahojiwa. Yupo
ndani, sisi tunaendelea kumsubiri nje,” amesema Marto.
Mwenyekiti
huyo alizungumza na Mwananchi kupitia simu ya mbunge huyo na kubainisha
kwamba mpaka wakati huo (saa 12:30 jioni) jeshi hilo halikubainisha
sababu za kumshikilia Msigwa.
“Alikuwa
na kibali cha kufanya mkutano katika kata tatu kuanzia leo Jumapili
mpaka Jumanne. Alianza kuzungumza saa tisa alasiri ilipofika saa 11:24
jioni, RCO akiwa na polisi wengi wakamshusha jukwaani na kuondoka naye,”
alisema Marto bila kufafanua sababu za kukamatwa.
CHANZO: MWANANCHI
CHANZO: MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment