Na Erasto Chin’goro WAMJW
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Bibi
Sihaba Nkinga amewahamasisha wananchi kujitolea katika kutekeleza
shughuliza maendeleo ikiwa ni sehemu ya kuhamsha ari wananchi kufanya
kazi za maendeleo yao.
Ameyasema
hayo katika ziara yake Mkoani Iringa wakati katika jitihada zake za
kuhakakisha jamii inahuisha ari ya kushiriki shughuli za kujitolea na
uanzishaji wa miradi inayoibuliwa na kutekelezwa na wananachi wenyewe
kwa kushiriki kazi mbalimbali za utekelezaji wa shughuli hizo katika
maeneo ya mijini na vijijini.
“Dhana
ya maendeleo ya jamii inawataka wananachi kujitolea kushiriki kazi za
maendeleo kwa kushirikisha kubaini mahitaji na changamoto
zinazowakabaili wananachi na kujadiliana pamoja kuhusu mbinu za utatauzi
wa changamoto hizo” alisema Bibi Sihaba.
Bibi
Sihaba ameongeza kuwa wananchi waendelee kuainisha ushiriki wao katika
kukamilisha miradi hiyo ya pamoja kwa kutumia rasilimali na nguzu kazi
ya ndani badala ya kutegemea misaada ya nje ya jamii.
Aidha Katibu Mkuu Bibi Sihaba Nkinga amewataka wananchi katika maeneo mengine kuiga mfano bora wa kijiji cha Ufyemba ili kujiletea maendeleo bila kusubiria msaada wa Serikali kuu.
Dhana hii ya kujitolea katika kutekeleza shughuli za maendeleo imefanikisha kijiji
cha Ufyemba kata ya Wasa kilichoko wilaya ya Iringa vijijini, mkoani
Iringa kushirikiana na wananchi kukamilisha ujenzi wa zahanati ili
kupata uhakika wa huduma za afya kwa watoto, wanawake, na jamii kwa
ujumla.
Katika tukio hili, Katibu Mkuu aliongozana na uongozi wa mkoa wa Iringa ukiongozwa na KAtibu tawala Mkoa wa Iringa Bibi Wamoja Ayoub, viongozi wa wilaya ya Iringa vijijini, uongozi wa kata ya Wasa na kijiji cha Ufyemba.
0 comments:
Post a Comment