Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu
wa wilaya ya Kilolo Asia Abdallah akizungumza wakati wa uzinduzi wa
mitandao wa TTCL 4G LTE katika Mkoa wa Iringa eneo la ofisi za kampuni
hiyo.
Mkuu
wa wilaya ya Kilolo Asia Abdallah akizindua huduma ya mtandao wa simu
wa TTCL kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa bi Amina Masenza
Picha ya Pamoja.
Na fredy Mgunda, Iringa.
Watanzania wametakiwa kuanza kuutumia mtandao wa simu wa TTCL kwa kuwa umeboreshwa kwa kiwango kikubwa na huduma zao zinazingatia wateja wake ili kuendelea kiinufaisha serikali kwa kuwa mtandao huo unamilikiwa na serikali.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa TTCL 4G mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah alisema kuwa wananchi wanapaswa kuunga mkono mtandao huu wa kizalendo ambao unahuduma nyingi nzuri.
“Ukiangalia utagundua kuwa mtandao wa TTCL inahuduma ya pesa ambazo zina makato madogo sana kulinganisha mitandao mingine hivyo nawasiii wananchi wa mkoa wa iringa kuanza kutumia huduma za mtandao huu wa kizalendo” alisema Abdallah
Abdallah aliwataka wananchi kuanza kuvithamini vitu vya wazawa kwanza ili kuleta maendeleo ya maendeleo kwenye kampuni na taasisi za kizalendo ndio maana mkuu wa mkoa wa Iringa na wakuu wa wilaya wote wa mkoa huu wameamua kujiunga na mtandao huu wa TTCL.
“Mimi,mkuu wa mkoa ,mkuu wa wilaya Richard Kasesela na viongozi wengine wamejiunga na mtandao huu wa TTCL 4G ambao unakasi kubwa kwenye upande wa internet na huduma nyingine ziboreshwa na zimekuwa bora sana” alisema Abdallah.
0 comments:
Post a Comment