Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Balozi
wa Japani nchi Tanzania, Masaharu Yoshida akikata utepe wakati wa
uzinduzi wa Bweni la wanafunzi wa shule ya sekondari ya Idodi mkoani
Iringa. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bibi Amina Masenza.
Balozi
wa Japani nchi Tanzania, Masaharu Yoshida akiwa amevalishwa vazi la
heshima la wazee wa kabila la Kihehe baada ya kuwezesha ujenzi wa Bweni
la Wasichana wa shule ya sekondari ya Idodi mkoani Iringa. Kushoto kwake
ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi na Mkuu
wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela.
Balozi
wa Japani nchi Tanzania, Masaharu Yoshida akiwa amevalishwa vazi la
heshima la wazee wa kabila la Kihehe baada ya kuwezesha ujenzi wa Bweni
la Wasichana wa shule ya sekondari ya Idodi mkoani Iringa. Kushoto kwake
ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi na Mkuu
wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Idodi wilaya ya Iringa Mkoani Iringa.
Jengo la Bweni la Wasichana wa shule ya sekondari ya Idodi mkoani Iringa kwa mbele.
Jengo la Bweni la Wasichana wa shule ya sekondari ya Idodi mkoani Iringa kwa nyuma.
Jengo la Bweni la Wasichana wa shule ya sekondari ya Idodi mkoani Iringa kwa ndani.
Vitanda
kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya sekondari Idodi ndani ya Jengo la
Bweni la Wasichana wa shule ya sekondari ya Idodi mkoani Iringa.
Vitanda
kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya sekondari Idodi ndani ya Jengo la
Bweni la Wasichana wa shule ya sekondari ya Idodi mkoani Iringa.
Eneo la kunawia lililo ndani ya Jengo la Bweni la Wasichana wa shule ya sekondari ya Idodi mkoani Iringa.
Na Hassan Mabuye
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi ambaye ni Mbunge
wa Jimbo la Ismani Mkoani Iringa kwa kushirikiana na Ubalozi wa Japan
amesaidia ujenzi wa bweni la wanafunzi katika shule ya sekondari Idodi
wilaya ya Iringa Mkoani Iringa kwa kiasi cha shilingi milioni 270.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa Bweni la wanafunzi wa shule ya sekondari ya Idodi
Iringa Balozi wa Japani nchi Tanzania, Masaharu Yoshida alisema kuwa
misaada hiyo inatolewa kupitia kodi za watu wa Japan kwa ajili ya kuunga
mkono shughuli za kimaendeleo nchini Tanzania.
Ubalozi
huo wa Japan ambao umesaidia ujenzi wa bweni la wanafunzi katika shule
ya sekondari Idodi umetokana na maombi ya mbunge wa Jimbo hilo la
Isimani Mhe. Wiliam Lukuvi aliyoyaomba katika ofisi ya ubalozi kufuatia
bweni la awali la shule hiyo kuteketea kwa Moto.
Balozi
huyo alisema kuwa mkataba wa ujenzi wa bweni hilo la wanafunzi Idodi
sekondari ulisainiwa February mwaka 2016 kwa dolla za kimarekani 130,166
sawa na milioni 270 za kitanzania kwa ajili ya ujenzi wa bweni hilo.
Ubalozi
wa Japan nchini Tanzania umeahidi kuendelea kusaidia miradi mbali mbali
ya kimaendeleo ndani ya mkoa wa Iringa na maeneno mengine hapa nchini
ili kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt
John Magufuli.
“waziri
Lukuvi lileta maombi ya miradi mbalimbali ambayo miongoni mwake ni
kujengewa Hostel ya wasichana ya shule ya Ismani ambayo ilijengwa toka
mwaka 2005 na mwaka 2008, kujenga jengo la OPD na wodi ya wagonjwa
katika zahanati ya Mlowa na mwaka 2010 kununua gari la wagonjwa katika
zahanati ya Mlowa, kwa hiyo namshukuru Waziri Lukuvi kwa kusimamia vema
miradi hiyo”
“Leo
nimefurahi kuona ujenzi umekamilika kwa kiwango kizuri vitanda vya
kutosha, mfumo wa kuhifadhi maji wa Hosteli hii umekamilika ikiwa na
uwezo wa kulaza wanafunzi 208 kama kusudio la ujenzi, na ni matumaini
yangu mradi huu utatunzwa vema”
Balozi
huyo alisema kutokana na usimamizi mzuri walioufanya kampuni ya Koyo
Corporation kampuni ya kijapani imetoa msaada wa taa zinazotumia nguvu
ya mionzi ya jua kwa ajili ya kutumia wanafunzi wote watakaoishi katika
bweni hilo.
Hata
hivyo alisema ubalozi wa Japan nchini utaendelea kuunga mkono jitihada
za serikali ya Tanzania chini ya kauli mbiu ya hapa kazi tu.
Mkuu
wa mkoa wa Iringa Amina Masenza awali akimkaribisha balozi huyo alisema
kuwa serikali ya mkoa inafurahishwa na msaada huo ambao umesaidia
kupunguza msongamano ya wanafunzi bwenini na hivyo bweni hilo ambalo
litatunzwa vizuri.
Waziri
Lukuvi pamoja na kupongeza msaada huo wa kujengewa bweni na miradi
mingine amewataka wanafunzi hao kutunza mabweni hayo na kujiepusha na
hatari zozote za kuchoma moto, kitendo ambacho kinasababisha upotevu
mkubwa wa mali na uhai wa wanafunzi hao.
0 comments:
Post a Comment