Hatua hiyo imekuja baada ya maofisa wa TRA kufanya ukaguzi wa
kushitukiza katika maeneo mbalimbali ya mji wa Iringa na kubaini uwepo
wa wafanyabiashara wanaodaiwa kutokuwa na mashine za kutolea risiti za
EFD.
Meneja wa TRA Mkoa wa Iringa, Ndg Lampson Tulianje amesema
wafanyabishara hao wamekaidi agizo la Serikali la kutakiwa kuwa na
mashine kwa zaidi ya miezi mitatu.
“Tumewapa maagizo, tumewahamasisha kwa zaidi ya miezi mitatu
lakini bado wamekaidi agizo letu, uamuzi tuliochukua ni kufunga duka na
mara atakaponunua tunamfungulia duka lake,”amesema Tulianje .
Tulinje amefafanuaa kuwa lengo la kufikia hatua hiyo ni kuhimiza
wafanyabiashara hao kulipa kodi stahiki kwa kutumia mashine hizo ambazo
zina uwezo wa kuweka kumbukumbu vizuri za mauzo ya bidhaa zao.
Pia Tulinje ametoa wito kwa wafanyabiashara hao kuacha kushindana na
Serikali badala yake kuhakikisha wananunua mashine hizo na kuzitumia kwa
kuwa hata gharama wanazotumia zinarudishwa na TRA wakati wa kukadiria
kodi zao.
“Rai kwa wafanyabiashara ni vyema wakanunua mashine
zitakazosaidia kuweka vizuri kumbukumbiu za mauzo yao na kuisaidia
Serikali kukusanya kodi sahihi, zaidi yote mashine hizo zinatolewa bure
na TRA kwa kuwa gharama wanazotumia kununulia mashine zitaunganishwa
kwenye makadirio ya kodi yao ya mapato,”amesema Tulianje kwenye mahojiano yake na Gazeti la Mwananchi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabishara mkoani
Iringa, Ndg Odilo Ngamiraga amesema wafanyabishara hawajagoma kutumia
mashine hizo na kwamba tatizo lipo kwa wasambazaji ambao pindi
wanapokwenda huambiwa wasubiri.
0 comments:
Post a Comment