Home » » RC IRINGA AMPONGEZA SALIM ABRI ASAS KUSAIDIA KUOKOA MAISHA YA MAJERUHI WA AJALI

RC IRINGA AMPONGEZA SALIM ABRI ASAS KUSAIDIA KUOKOA MAISHA YA MAJERUHI WA AJALI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Mwenyekiti  wa kamati ya  usalama barabarani mkoa wa Iringa Salim Abri  Asas (kushoto) akimkabidhi  mgeni  rasmi katika maadhimisho ya  wiki ya nenda kwausalama kwa mkoa wa Iringa leo , mkuu wa mkoa wa Iringa Amina  Juma Masenza zawadi maalum  ya kamati ya usalama barabarani  mkoa kutokana na mchango  wake mkubwa kwa kamati   hiyo
Kitengo cha  usalama barabarani mkoa wa  Iringa  wakijiandaa kutoa elimu katika  viwanja vya maadhimisho ya  wiki ya nenda kwa   usalama barabarani
Baadhi ya  wananchi na  watu  wenye  ulemavu  wakiwa  katika  viwanja  vya maadhimisho  hayo
Mwakilishi wa  wakala  wa barabara mkoa wa Iringa  akitoa maelezo kwa mkuu wa mkoa wa Iringa na watu mbali mbali  waliotembelea banda hilo  kuona shughuli  zinazofanywa
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Juma Masenza  akitoa  hotuba yake  leo  wakati wa maadhimisho ya  wiki ya nenda kwa  usalama barabarani ,kulia kwake ni mwenyekiti wa kamati ya  usalama barabarani mkoa wa Iringa Salim Abri Asas na katibu  wake RTO Leopold Fungu wakifuatilia hotuba   hiyo
Mkuu  wa  mkoa wa  Iringa Amina Juma Masenza akihamasisha  upimaji afya na uchangiaji damu katika  banda la HOspitali ya Rufaa mkoa wa Iringa ambao  walishiriki maadhimisho hayo ya wiki ya  nenda kwa usalama mkoa wa Iringa leo kwenye viwanja vya stendi kuu ya mkoa
Mkuu  wa  mkoa wa Iringa Amina Juma Masenza (wa tatu kushoto  waliokaa) akiwa  katika  picha ya pamoja na wadau na kamati ya usalama barabarani mkoa wa Iringa mara baada ya kumalizika  kwa maadhimisho hayo katika  viwanja vya Stendi kuu , kushoto kwake ni katibu  tawala wa mkoa wa Iringa Wamoja  Ayubu ,Kaimu RPC , DC Iringa Richard Kasesela ,Naibu  meya  wa Manispaa ya Iringa Mh. Lyata  na kutoka kushoto wa kwanza ni katibu wa kamati ya usalama barabarani mkoa Leopold Fungu na mwenyekiti  wake  wa kamati  Salim Abri Asas
Dc Iringa Richard Kasesela akipata  maelezo katika  banda la  zima moto
Afisa  habari  mkoa wa Iringa  Denis Gondwe akipokea maelekezo toka kikosi cha usalama barabarani
Mkuu  wa  mkoa wa Iringa Amina Juma Masenza akiwa akishirikiana na mwanafunzi  wenye ulemavu wa ngozi toka Lugalo  sekondari  Semeny  Sadick  kuzima moto  uliowashwa na kikosi cha zimamoto na uokoaji ili  kutoa  elimu kwa  wananchi  juu ya uzimaji moto baada ya  kikosi hicho  kutoa elimu katika  shule  zote za Manispaa ya Iringa
Mwanafunzi  Semeny  akizima  moto
Wasanii  toka Mkwawa Magic Site Iringa wakionyesha ujuzi  wa  kucheza  na nyoka aina ya chatu
Askari  wa usalama barabarani  mkoa wa Iringa maarufu kwa jina la bibi akimpa  pesa  msanii  wa Mkwawa Magic Site 
Msanii  toka kikundi  cha Mkwawa Magic Site  akicheza  mbele ya mgeni rasmi

Na MatukiodaimaBlog
MKUU  wa  mkoa  wa  Iringa  Amina  Masenza ameipongeza  kazi  kubwa  inayofanywa na kamati ya  usalama  barabara  mkoa  wa Iringa  chini ya  mwenyekiti wa kamati hiyo Salim  Abri Asas  ambae  amekuwa ni msaada mkubwa katika  kuokoa maisha ya  watanzania  wanaopata ajali ndani ya mkoa  kwa kujitolea misaada  mbali mbali  ikiwemo ya dawa na usafiri.

Akitoa  pongezi  hizo  leo  wakati wa maadhimisho ya wiki ya nenda  kwa usalama ambayo  imeadhimishwa  kimkoa katika viwanja  vya  stendi  ya mabasi yaendayo  mikoani mjini Iringa ,mkuu  huyo wa mkoa alisema  mbali ya  kuwepo kwa  wadau mbali mbali katika kupunguza ajali na kusaidia pindi ajali  zinapotokea  ila serikali yake  ngazi ya  mkoa inatambua mchango mkubwa  unaotolewa na familia  ya mfanyabiashara  Asas  katika  kusaidia  kuokoa roho za  watanzania  pindi  wanapopatwa ajali.

“ Kana mambo  mengi makubwa ambayo Asas amekuwa  akijitolea  kuyafanya kwa ajili ya  kunusuru maisha ya majeruhi  wanaopatwa na ajali  ndani ya  mkoa  wetu  mfano katika ajali  iliyotokea Changalawe Mafinga kwa  kuhusisha basi la Majinja  ajali  iliyoua  watu  zaidi  ya 50 na kujeruhi  wengine  wengi …msaada mkubwa  wa  kuokoa roho za majeruhi  kwa  kujitolea dawa zilionyeshwa na Asas ….mimi nikiwa ni mkuu wa mkoa na  serikali ya  mkoa tunapongeza kazi  nzuri ya  Asas  na familia  yake katika  kuwaidia  kuokoa roho za  majeruhi naomba  Mwenyezi Mungu azidi  kumuongezea pale anapopunguza kwa  ajili ya wengine”

 Alisema  kuwa wiki ya  nenda kwa  usalama  ni kwa ajili ya  kukumbushana  mema yanayohusu  kufuata  sheria  na kanuni  za usalama  barabarani ili  kuondoa vifo  vinavyotokana na ajali barabarani   hivyo  pamoja na kumbushana kanuni  na sheria za usalama barabarani ni  vema  kutumia  maadhimisho hayo  kutambua  michango  mbali mbali ya wadau  wanaojitolea kwa jili ya kufanikisha  elimu ya usalama bararani ama kusaidia kuokoa majeruhi na vinginevyo.

“ Kumekuwepo na ongezeko  kubwa la ajali  za  barabarani zinazohusisha  pikipiki  ajali hizi  zinaweza  kuepukika endapo  waendesha  na wapanda pikipiki watazingatia  sheria  na kanuni  za usalama barabarani ….natoa  wito  kwa  wapanda pikipiki kuacha  tabia ya  kuendesha bila kupata mafunzo na kutokuwa na leseni  suala la  kuvaa kofia  ngumu kwa madereva na abiria ni lazima …..acheni tabia ya kubeba abiria  zaidi ya mmoja (mshikaki) …..pia  kuacha kunywa  pombe  vikiwemo  viroba wakati wa  kutoa  huduma ya  usafiri …..kweli naumia sana kuona  vijana  wanakufa baada ya  kuendesha  pikipiki huku  wakiwa wamelewa  viroba”alisema mkuu  huyo wa  mkoa 

Kwa  watumiaji wengine wa barabara ni  vema kuzingatia  sheria  za  usalama barabarani  kwa  kufunga  mikanda  pindi  wanapokuwa katika magari  pia abiria  kuacha  kushabikia mwendo kasi na badala yake  kuwafichua madereva  wanaokiuka  sheria za usalama barabarani.
Hata   hivyo  mkuu   huyo wa  mkoa  aliagiza  jeshi la polisi  kikosi cha usalama  barabarani  kuwakamata  waendesha  boda boda   wote  wanaoendesha  boda boda  kwa vurugu  na baadhi yao  kushitua  watu kwa  kuifanya boda boda   hiyo  kutoa mlio mkali mfano wa bomu .

Aidha alitaka  kuanzia  sasa  dereva  boda  boda  atakayebainika kusababisha ajali na  kuita  wenzake kwa  ajili ya  kumfanyia vurugu aliyesababishiwa ajali  kukamatwa na  washiriki  wake na kufikishwa mahakamani .

Kwa upande  wake  mwenyekiti wa  kamati ya  usalama  barabarani  mkoa  wa Iringa Salim Abri  alisema  kuwa  kuna  dhana  potofu kwa  baadhi ya  watu  kufikiri suala la  usalama  barabarani  linahusu ajali  pekee yake kwani hata  kupiga  honi bila  sababu ama  kukwamisha shughuli za barabara kwa  mambo  binafsi  pia ni kero  kwa  watumiaji  wengine wa  barabara .

“Tunapozungumzia  sheria za  usalama barabani  sit u kwa ajili ya  kuepusha ajali ila  ni pamoja na kuepusha  kero  za  usalama barabarani baadhi  yetu  tumekuwa  tukifikiri usalama barabarani ni kuepusha ajali  tu ila ukweli ukizingatia  usalama barabarani ni pamoja na kero kubwa ya kutozingatia  sheria  za  usalama barabarani hata  kupiga  honi bila  sababu ni  kero…..”

Alisema   katika  watumiaji wa  vyombo  vya  moto  wanaoongoza kwa  kuvunja sheria  za usalama barabrani na kero  nyingine za  barabarani ni boda  boda   hivyo angependa  kuwaomba  waendesha  boda boda  kupunguza  kero za  usalama barabarani zikiwemo za  kupiga  honi ovyo na ajali zinazoweza   kuepukika .

Katibu  wa kamati  ya  usalama  barabarani  mkoa  wa  Iringa  ambae ni mkuu wa kikosi  cha usalama barabarani mkoa (RTO) Leopold Fungu  alisema  kuwa  kwa  mujibu  wa tathimini ya jail  za barabarani kwa  kipindi  cha miezi tisa  mwaka 2015 ikilinganishwa na kipindi kama hicho  cha mwaka huu 2016 mkoa  wa  Iringa  umefanikiwa kwa  kiasi kikubwa  kupunguza ajali  za  barabarani .

Kuwa kwa kipindi cha  January  hadi Septemba mwaka 2015 ajali  zilikuwa ni 41 ila  kwa  kipindi  cha January  2016 hadi  septemba 30  ni  ajali 35   ndizo  zilizotokea  wakati  watu  waliopoteza maisha kwa kipindi  cha January 2015 hadi Septemba  ilikuwa ni 34  ila kwa  mwaka  huu toka  January hadi Septemba 30  ni  watu 30 ndio  waliopoteza maisha  aidha katika  kipindi  hicho ajali  za  piki piki  zimepungua kwa asilimia 15 huku  watu  waliokufa kwa ajili ya  pikipiki wamepungua kwa asilimia 11 na waliojeruhiwa wamepungua kwa asilimia 20 kuwa  kupungua kwa matukio ya ajali ni  kutokana na elimu za mara kwa mara.

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa