Home » » RC IRINGA NA CHADEMA JICHO KWA JICHO YEYE APIGA MARUFUKU OPARESHENI UKUTA , CHADEMA WASEMA WANASUBIRI MUDA

RC IRINGA NA CHADEMA JICHO KWA JICHO YEYE APIGA MARUFUKU OPARESHENI UKUTA , CHADEMA WASEMA WANASUBIRI MUDA

Mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa Bi  Amina  Masenza  akisikiliza  maswali ya wanahabari kuhusu sababu  za   serikali  kuzuia vyama  kufanya mikutano
Baadhi  ya wataalam  ofisi ya  RC  Iringa na  wanahabari  wakiwa katika mkutano wa pamoja na wanahabari  leo
Baadhi ya  wakuu wa Idara  ofisi ya RC  Iringa  wakiwa katika mkutano wa pamoja kati ya RC  na  wanahabari leo

RC  Iringa akisubiri maswali
Baadhi ya  wanahabari  wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Iringa
Na MatukiodamaBlog

WAKATI  chama    cha  Demokrasia  na maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (Nyasa) kikitangaza kikijiandaa kwa utekelezaji wa azimio ya  kamati  kuu  cha Chadema  chini ya mwenyekiti  wake   Taifa   Bw  Freeman  Mbowe  kwa kujipanga kwa   oparesheni  UKUTA ,mkuu  wa  mkoa wa  Iringa Bi  Amina Masenza (pichani)amepiga marufuku maandamano ya  vyama  vya siasa  wala viongozi wageni  kutoka nje ya mkoa  wa Iringa kufanya mikutano ndani ya mkoa  huo.

Mkuu  huyo  wa mkoa  aliyasema hayo jana  wakati akizungumza na  wanahabari  ofisini  kwake  kuhusiana na utekelezaji wa ilani ya CCM na utekelezaji  wa agizo la Rais Dr  John Magufuli la kuzuia maandamano na mikutano ya  kichochezi nchini.

" Mikutano  inayoruhusiwa ni ile  ya madiwani na  wabunge  katika majimbo  yao .....hivyo naomba  kuelekewa sitakubali  kuona maandamano wala  viongozi wa vyama vya  kisiasa  kutoka nje ya majimbo ama kata   husika  kuja  kufanya mikutano ama maandamano katika jimbo ama kata  nyingine"

Mkuu  huyo  wa  mkoa alisema kuwa hakuna  diwani  wala  mbunge ambaye amezuiliwa  kufanya mikutano ya  kimaendele katika eneo lake na  kuwa mikutano inayozuiwa ni ile ya vyama  vya siasa ambayo  kimsingi muda  wake bado haujafika na  pindi muda wa siasa ukifika  vyama vitaruhusiwa  kufanya  siasa  ila kwa sasa ni  wakati wa kufanya kazi za  kuwaletea  wananchi  maendeleo.

" Kila jambo  linawakati  wake suala la siasa lilimalizika baada ya  uchaguzi  mkuu na  tayari  madiwani  ,wabunge na  Rais amekwisha patikana kinachoendelea  sasa ni  wale  waliochaguliwa  kuwatumikia  wananchi kwa kufanya kazi  si vinginevyo "alisisitiza  mkuu  huyo wa mkoa 

kuwa katika kata  zote  na majimbo yote  ya mkoa  wa Iringa angependa  kuona  wanaofanya  mikutano ya  kimaendeleo ni wahusika  wa maeneo hayo na sio watu  kutoka nje ya maeneo  husika .

Katika  hatua  nyingine  mkuu  huyo wa mkoa wa Iringa alisema  kuwa hata madiwani na  wabunge ambao  wameruhusiwa  kufanya mikutano ya  kimaendeleo katika maeneo yao ,serikali ya  mkoa huo haitawavumilia wale  wote  watakaotumia vibaya nafasi hiyo  kwa  kutukana amakumsema  vibaya Rais ama  chama  kingine cha  siasa .

Bw Frank  Mwaisumbi
Zuio  hilo la mkuu  wa mkoa wa Iringa limekuja  huku ikiwa ni siku tatu toka Chadema kanda ya nyanda  za  juu kusini (nyasa) kutoa taarifa kwa  vyombo  vya habari  kuunga mkono azimio la kamati kuu ya chadema kupanga kuanza oparesheni UKUTA Septemba mosi mwaka huu .

Katika taarifa  yake kwa vyombo  vya habari katibu  wa  kanda   ya nyanda  za  juu  kusini Bw  Frank  Mwaisumbe alisema  wamepokea  kwa mikono  miwili maamizimio  hayo  ya  kuanzisha  oparesheni  UKUTA  nchini  nzima  na  kuwa wapo  tayari  kwa  kushiriki .

“Kwa ujumla wake (Mkoa wa Mbeya, Songwe, Rukwa, Iringa na Njombe) inaunga mkono maazimio ya Kamati kuu ya Chama Chetu iliyoketi tarehe 27/07/2016 ya kupinga vikali aina zote za udikteta zinazoendelea na kufanywa na serikali ya chama cha Mapinduzi (CCM)….. na kuwa tupo tayari kuona Demokrasia ya  vyama vingi  nchini Tanzania inaendelea  kuimarika kama  iliyo asisiwa na Baba wa Taifa Mwal. Julius kamabarage Nyerere, ambayo aliiacha ikiwa na amani na utulivu na kuwa nchi yenye kuruhusu mfumo wa vyama vingi”

Alisema  kuwa  kwa  kuwa Tanzania  ni  moja kati ya  nchi zinazoendeshwa  kwa mfumo  wa  vyama  vingi  ni  vema  chama  tawala CCM  kuacha  kufinyanga  Demokrasia hiyo na  kuviacha   vyama  vyote  kufanya  kazi ya   kujiimarisha  kwa  uhuru na amani  badala ya  kuzuia  vyama  kuendesha mambo  yao .

Kwani   alisema ili  chama  kiwe  imara  na  chenye  nguvu  ya  kuleta  ushindani ni   lazima  kuwekeza  kwa  wananchi  na hivyo kuanzishwa  kwa oparesheni UKUTA kutasaidia  Chama  chao  kuwekeza kwa  wananchi kazi  ambayo  hata   CCM wamekuwa wakiendelea  kuifanya  hadi  sasa .

Mwaisumbi alisema utakuwa ni  uonevu  mkubwa  iwapo  serikali ya  CCM itazuia  Chadema  kuendelea  na  Oparesheni  UKUTA   wakati juzi Dodoma katika  Uwanja  wa  Jamhuri aliyekuwa  mwenyekiti  wa CCM Taifa  Rais  Mstaafu  Dr  Jakaya  Kikwete  alifanya mkutano  mkubwa ambao  kimsingi si mkutano wa  kiserikali ila  ulikuwa ni mkutano wa Chama.

Alisema  siasa  safi  ni pamoja na kuruhusu vyama vyote  kuendelea ujenga  vyama vyao ikiwa ni pamoja na kutawaliwa na uhuru wa kuongea na uhuru wa kukosoa bila kuvunja katiba ya nchi.

Bw  Mwaisumbialisema  wao kama Chadema kanda ya Nyasa watahakikisha   wanafanya  zoezi hilo la Oparesheni  UKUTA pasipo kuvuruga  amani  ya  nchi na  kuona mikutano  yao  yote  inafanyika kwa uhuru na amani na  wapo  tayari  kuendelea   kulinda amani na utulivu.

“ sisi CHADEMA kanda ya Nyasa kwa pamoja tunajiunga na UKUTA Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania.. wa UKAWA na tupo tayari wakati wote kupambana na mtu yeyote anayevunja katiba na kuweka udikteta…. hii ni nchi yetu sote na tupewe uhuru kwa usawa bila kuvunja katiba ya nchi”



Wakati  huo  huo mbunge wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa katika  mkutano wake wa hadhara  alioufanya siku  moja kabla ya  mkuu wa mkoa wa Iringa  kupiga marufuku maandamano na  mikutano ya  wanasiasa  toka  nje ya kata na majimbo  husika ,alisema kinachofanywa na  serikali kupiga marufuku  mikutano ya  vyama ni kuua Demokrasia  nchini na kuwa suala  hili halitavumilika.

Mchungaji Msigwa alisema  kuwa  pamoja na kuwa mkutano  wake  huo ulikuwa wa jimbo kwa ajili ya maendeleo ila  pindi chama chake  kitakapo agiza kuanza kwa oparesheni UKUTA atawajulisha  wapiga  kura  wake .

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa