Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Rais
wa shirikisho la wachimbaji madini Tanzania (FEMATA ) Bw John Bina
akitambulishwa mbele ya balozi wa China nchini (hayupo pichani) kulia
ni waziri wa Kilimo ,Mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba
Bw John Bina akihamasisha uchangiaji wa madawati mashuleni
balozi wa Chini Nchini Tanzania Dr Lu Yonq.ng katikati akiwa na
viongozi wa mkoa wa Shingida kutoka kulia mkuu wa mkoa wa Singida Bw
Methew Mtigumwe,waziri
wa kilimo ,Mifugo na Uvuvi Bw Mwigulu Nchemba ,mbunge wa viti maalum
mkoa wa Singida Bi Martha Mlata na Rais wa FEMATA Bw John Bina
Na MatukiodaimaBlog ,
RAIS wa shirikisho la vyama
vya wachimbaji madini Tanzania (FEMATA) ametoa
wito kwa wachimbaji wote yakiwemo
makampuni makubwa ya uchimbaji wa
madini kujitokeza kumuunga mkono Rais Dr John Magufuli katika harambee ya kuchangia madawati kwa
shule mbali mbali hapa nchini.
Huku akisifu mwitikio mzuri wa kampuni ya Sunshine Minning kwa
kuunga kuitikia wito huo kwa kuchangia madawati 100 yenye thamani ya Tsh
milioni 85,000 kwa Halmashauri ya wilaya ya Iramba mkoani Singida .
Akizungumza na waandishi
wa habari jana ,Rais wa FEMATA John Bina alisema kuwa Shirikisho lake
limelazimika kumsaidia Rais Dr
Magufuli kuhamasisha uchangiaji wa madawati
kwa wanachama wake ili kumaliza kabisa tatizo hilo la uhaba
wa madawati na kuona sekta ya elimu nchini inaboresheka
zaidi kwa
kuhakikisha wanafunzi hawakai chini.
Bw Bina alisema kuwa
katika kuunga mkono jitihada za serikali wao kama sehemu
ya wadau wa maendeleo katika Taifa hawakupenda kuwa nyuma
kujitokeza kuchangia madawati hasa ukizingatia kuwa
elimu bora ni mwanzo wa kuwa na taifa bora .
"Suala hili la
elimu si la serikali pekee kila mmoja kwa nafasi yake ana umuhimu katika
kuboresha elimu nchini na si vema kwa
kila jambo kuitazama serikali ......serikali ina
nafasi yake ila na sisi wadau tuna nafasi yetu
katika kuiunga mkono serikali pia wanafunzi wananafasi yao
.... walimu na wazazi pia " alisema rais Bina
Hata hivyo
aliwataka wadau wengine na wananchi
mmoja mmoja kwa nafasi yake kujitokeza kuunga mkono uchangiaji wa
madawati ili kumaliza kabisa kero hiyo ya uhaba wa madawati
mashuleni.
Alisema wao kama wadau
wa maendeleo kupitia FEMATA wataendelea kuunga mkono
jitihada mbali mbali zinazoendelea kufanywa na serikali ya
Rais Dr Magufuli jitihada zenye lengo la kulifanya
Taifa kuzidi kuwa mbele kimaendeleo.
Pia
alisema kwa wadau wa
sekta hiyo ya madini pekee
kama kila mmoja atajitolea kuchangia madawati upo
uwezekano mkubwa wa zoezi hilo kukamilika mapema zaidi na kuwataka wadau
wengine mbali ya wale wa
madini nao kwa nafasi zao
kujitolea madawati badala ya kuiachia
serikali pekee.
“ Ninakusudia kama
Rais wa FEMATA kuwakutanisha
wachimbaji wote mbali na mambo
mengine tutaangalia ushiriki
wetu katika masuala ya kijamii
yakiwemo ya uchangiaji wa madawati”
Hata hivyo mkuu
wa mkoa wa
Singida Bw Methew Mtigumwe mbali ya
kupongeza harakati za Rais huyo wa FEMATA kwa
kuunga mkono agizo la rais kwa
kujitolea kuhamasisha uchangiaji
wa madawati bado alisema
kuwa jambo hilo ni jema na linapaswa kupongezwa zaidi.
Alisema katika mkoa wa Singida
kila mkuu wa wilaya
ameagizwa kusimamia utekelezaji wa agizo
la Rais la upungufu wa madawati katika eneo lake na kuwa mkoa umejipanga kumaliza kabisa kero
hiyo ya uhaba wa madawati .
MWISHO
KAWAIDA
RAIS
WA WACHIMBA MADINI AJITOSA RASMI KUMSAIDIA RAIS DR MAGUFULI ........
Rais wa shirikisho la wachimbaji madini Tanzania (FEMATA ) Bw John
Bina akitambulishwa mbele ya balozi wa China nchini (hayupo pichani)
kulia ni waziri wa Kilimo ,Mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba
Bw John Bina akihamasisha uchangiaji wa madawati mashuleni
balozi wa Chini Nchini Tanzania Dr Lu Yonq.ng katikati akiwa na
viongozi wa mkoa wa Shingida kutoka kulia mkuu wa mkoa wa Singida Bw
Methew Mtigumwe,waziri wa kilimo ,Mifugo na Uvuvi Bw Mwigulu Nchemba
,mbunge wa viti maalum mkoa wa Singida Bi Martha Mlata na Rais wa
FEMATA Bw John Bina
Na MatukiodaimaBlog ,
RAIS wa shirikisho la vyama vya wachimbaji madini Tanzania (FEMATA)
ametoa wito kwa wachimbaji wote yakiwemo makampuni makubwa ya
uchimbaji wa madini kujitokeza kumuunga mkono Rais Dr John Magufuli
katika harambee ya kuchangia madawati kwa shule mbali mbali hapa
nchini.
Huku akisifu mwitikio mzuri wa kampuni ya Sunshine Minning kwa
kuunga kuitikia wito huo kwa kuchangia madawati 100 yenye thamani ya
Tsh milioni 85,000 kwa Halmashauri ya wilaya ya Iramba mkoani Singida .
Akizungumza na waandishi wa habari jana ,Rais wa FEMATA John Bina
alisema kuwa Shirikisho lake limelazimika kumsaidia Rais Dr Magufuli
kuhamasisha uchangiaji wa madawati kwa wanachama wake ili kumaliza
kabisa tatizo hilo la uhaba wa madawati na kuona sekta ya elimu
nchini inaboresheka zaidi kwa kuhakikisha wanafunzi hawakai
chini.
Bw Bina alisema kuwa katika kuunga mkono jitihada za serikali wao
kama sehemu ya wadau wa maendeleo katika Taifa hawakupenda kuwa nyuma
kujitokeza kuchangia madawati hasa ukizingatia kuwa elimu bora ni
mwanzo wa kuwa na taifa bora .
"Suala hili la elimu si la serikali pekee kila mmoja kwa nafasi yake
ana umuhimu katika kuboresha elimu nchini na si vema kwa kila
jambo kuitazama serikali ......serikali ina nafasi yake ila na
sisi wadau tuna nafasi yetu katika kuiunga mkono serikali pia
wanafunzi wananafasi yao .... walimu na wazazi pia " alisema rais
Bina
Hata hivyo aliwataka wadau wengine na wananchi mmoja mmoja kwa
nafasi yake kujitokeza kuunga mkono uchangiaji wa madawati ili
kumaliza kabisa kero hiyo ya uhaba wa madawati mashuleni.
Alisema wao kama wadau wa maendeleo kupitia FEMATA wataendelea
kuunga mkono jitihada mbali mbali zinazoendelea kufanywa na serikali
ya Rais Dr Magufuli jitihada zenye lengo la kulifanya Taifa
kuzidi kuwa mbele kimaendeleo.
Pia alisema kwa wadau wa sekta hiyo ya madini pekee kama kila
mmoja atajitolea kuchangia madawati upo uwezekano mkubwa wa zoezi
hilo kukamilika mapema zaidi na kuwataka wadau wengine mbali ya
wale wa madini nao kwa nafasi zao kujitolea madawati badala ya
kuiachia serikali pekee.
“ Ninakusudia kama Rais wa FEMATA kuwakutanisha wachimbaji wote
mbali na mambo mengine tutaangalia ushiriki wetu katika masuala ya
kijamii yakiwemo ya uchangiaji wa madawati”
Hata hivyo mkuu wa mkoa wa Singida Bw Methew Mtigumwe mbali ya
kupongeza harakati za Rais huyo wa FEMATA kwa kuunga mkono agizo la
rais kwa kujitolea kuhamasisha uchangiaji wa madawati bado alisema
kuwa jambo hilo ni jema na linapaswa kupongezwa zaidi.
Alisema katika mkoa wa Singida kila mkuu wa wilaya ameagizwa
kusimamia utekelezaji wa agizo la Rais la upungufu wa madawati katika
eneo lake na kuwa mkoa umejipanga kumaliza kabisa kero hiyo ya uhaba
wa madawati .
MWISHO
0 comments:
Post a Comment