Na Zawadi Msalla- Iringa.
Wanahabari
wa Mkoa wa Iringa wameeleza masikitiko
yao ya ukosefu wa Mikataba ya ajira ambayo
inasababisha upotevu wa haki zao za msingi katika utekelezaji wa
majukumu yao ya kila siku.
Wakieleza
masikitiko hayo mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na
Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel jana
alipotembelea mkoa huo kujionea shughuli mbalimbali za kisekta za Wizara hiyo
walisema ni kwakipindi kirefu sasa tatizo hiloni kilio chao.
Wadau
hao wa habari walidai kukosekana kwa mikataba ya kazi imekuwa ni kikwazo
kikubwa kinacho wakatisha tamaa na hivyo
kuitaka Wizara iangalie kwa umakini suala hilo na kuliingiza katika sheria
tarajiwa ya habari.
Akiwakilisha maoni yake Bwana Leonard Frank alisema
waandishi wengi wanategemea bahasha katika kuendesha maisha yao ya kila siku
kwakuwa hawana mikataba ya ajira hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa maisha ya
wana habari kuwa duni.
“Hakuna
mishahara,Malipo stahili sawasawa na kazi zetu wala maslahi nyingine
zozote”alisema.
Aidha
waliiomba Serikali kuangalia namna ya kukaa na wamiliki wa vyombo vya habari
ili kuweza kujadili suala hilo na kutafutia ufumbuzi wa kudumu.
Naye
Katibu Mkuu akijibu hoja hiyo aliwataka wamiliki wa vyombo vya Habari wasisubiri
mpaka sheria mpya ya habari itoke iliwaweze kutatua suala hilo kwani ni haki ya
msingi ya mtu yeyote anaye fanya kazi.
Alisisitiza
kuwa kulipa vizuri waandishi wa habari itasaidia waandishi kufanya kazi kwa
moyo na kukuza vyombo vyao.
“Sheria
isishurutishe watu, haki ya msingi ya kibinadamu lazima ibaki kuwa haki ya
msingi kama kweli wamiliki mnahitaji matokeo mazuri zingatieni suala zima la
mikataba”Alisema Profesa Gabriel.
Pia
aliwataka waandishi wa habari wajiweke vizuri ili thamani yao ionekane na
kuongeza kuwa imefika wakati wa waandishi kuhakikisha jamii inatambua kuwa bila
uwepo wao mambo hayawezi kwenda vizuri.
“Hakuna
atakaye kuthamini kama hauoneshi kwanini una umuhimu wa kuwepo hapo, kama
mwajiri wako haoni tofauti ya uwepo wako au kutokuwepo kwako basi haina haja ya
kulilia mkataba” Aliongeza Profesa Gabriel.
Aliwaambia
Wizara yake ipo katika mkakati wa kuinua sekta zake nne ili ziweze kutambulika
na kuonekana katikati ya jamii.
0 comments:
Post a Comment