Home » » MKUTANO WA KUJADILI UPANGAJI WA MIPANGO WA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA

MKUTANO WA KUJADILI UPANGAJI WA MIPANGO WA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Iringa, Martin Mlwafu akifungua mkutano wa kujadili upangaji wa mipango ili kuboresha upatikanaji wa huduma bora za afya katika halmashauri ya wilaya ya Iringa uliofanyika mjini Iringa leo.
Afisa Uchechemuzi (Advocacy Strategies) kutoka TACOSODE, Abraham Kimuli akifafanua jambo wakati mkutano.

Mkutano huo wenye madhumuni ya kushirikiana katika matokeo ya utekelezaji wa mradi wa CEGO (citizens engaging in government oversight in health service provision ) kwa kupitia mfumo wa ufuatiliaji wa uwajibikaji jamii (social accountability monitoring-SAM ).

Mradi huo unatekelezwa na TACOSODE kwa ufadhili wa watu wa marekani (USAID).

Mkutano huo pia unatoa fursa ya kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya afya na kuadhiri kwa kiasi fulani upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wananchi wa halmashauri hiyo.
Secretarieti kutoka TACOSODE wakifuatilia majadiliano.
Washiriki wakifuatilia kwa umakini
Makamu Mwenyekiti wa TACOSODE, Leonard Lugenge akitoa maneno ya utangulizi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi. 

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa