Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Kamanda wa UVCCM Mkoa Salim Asas akiwa na aliyekuwa Mgombea Ubunge jimbo la Iringa Mjini Balozi Augustino Mahiga leo ofisi za CCm Wilaya
Makada wa CCM
Balozi Mahiga akipokelewa
MWAKALEBELA Mgombea Ubunge akipokelewa
Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Iringa Monica Mbega akipokelewa
Balozi Mahiga
Aliyekuwa Naibu Katibu mkuu ambae leo mgeni RASMI Bw Nchemna akiwasili
Mwakalebela katikati akiwa na mwigulu Kushoto kuelekea uwanja wa Mwembetogwa
Baadhi ya wasanini wa Bongo Muvi wakiwa jukwaani |
Mwakalebela akiomba kura
Mwigulu akiomba kura za CCM wakati wa uzinduzi wa kampeni za Ubunge jimbo la Iringa Mjini leo
Wananchi wakiwa juu ya miti baada ya uwanja kujaa
Kada maarufu wa CCM Bw Fahad Abri ambae ni Mdau wa wanahabari Mkoa wa Iringa na kiongozi wa mtandao wa matukiodaima akiwa katika mkutano
Mumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa ARIF Abri mwenye kanzu katikati ,Katibu wa CCM Mkoa Bw Mtenga , Kamanda wa Uv CCM Salim Asas wakifuatilia mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM
Na MatukiodaimaBlog ,Iringa
CHAMA
cha mapinduzi ( CCM ) jimbo la Iringa Mjini wazindua mkutano wa kampeni
za Ubunge kwa kushindo huku Naibu Katibu mkuu mstaafu CCM Mwigulu
Nchemba azindua kampeni za Ubunge jimbo la Iringa Mjini kwa kumnadi
Frederick Mwakalebela huku akiwataka wananchi kuchagua mtu wa kwenda
kufanya Kazi ikulu ya kuwatumikia wananchi na sio wa kwenda kujaza
nafasi inayoachwa wazi na Rais Dr Jakaya Kikwete
Mwigulu
ambae alikuwa mmoja Kati ya Makada wa CCM waliojitokwza kuwania Urais
pamoja na Dr John Magufuli na Naibu Waziri wa fedha aliyasema hayo jana
wakati akizundua kampeni hizo za CCM jimbo la Iringa Mjini katika uwanja
wa Mwembetogwa.
Alisema
kuwa Kati ya wagombea wa Urais wa Vyama vyote vya siasa hapa nchini na
wale waliojitokeza kuwania nafasi hiyo ndani ya CCM hakuna hata mmoja
anaye mfikia Dr Magufuli kwa uadilifu na uchapakazi pamoja na
ufuatiliaji wa mambo na kuchukua hatua kwa wakati.
Bw
Mwigulu alisema kuwa Dr Magufuli hajazungukwa na watu wa dili wala
mtandao wa wakwepa kodi na kuwa mmoja Kati ya wagombea Urais toka Enzi
za baba wa Taifa alikuwa hana sifa ya kuwa kiongozi kutokana na kuwa ni
mtu wa kupiga dili kila sekta anayopewa.
"
Mgombea wa upande wa pili toka Enzi za Mwalimu alikuwa amezungukwa na
kuifanya Kazi ya kupiga dili kwenda mbele na sasa anataka kwenda
mwenyewe Ikulu kuendeleza kupiga dili ..... Leo tunataka kupeleka genge
la wapiga dili Ikulu .....tunasema hatuwezi kupeleka mpiga dili Ikulu "
Alisema kuwa mwaka huu watanzania wameanza kudanganywa na genge la wapiga dili ili kuwapeleka Ikulu jambo ambalo ni hatari .
Bw
Mwigulu akiwahutubia maelefu ya wakazi wa jimbo la Iringa ambao toka
kuanza kwa mfumo wa vyama vingi chama hicho hakijapata kupata idadi hiyo
ya watu ,alisema kuwa iwapo leo CCM wangemchukua mgombea wake Edward
Lowasa hali ingekuwaje ndani ya CCM.
Alisema
kuwa wapo ambao walikuwa wakipinga kwa nguvu zote Lowasa kuwa Rais
akiwemo mwenyekiti wa Chadema Taifa Bw Freeman Mbowe na aliyekuwa mbunge
wa jimbo la Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa ambao leo wamegeuka
kumtakasa waliyemwita fisadi ili awe Rais .
Aidha
alisema kuwa umefika wakati wa watanzania kuchukiwa watu wanaolazimisha
kupeleka Ikulu Rais wa kwenda kupumzika na kumuacha mtu wa Kazi Dr
Magufuli.
"
Ikulu wakati mwingine Baraza la mawaziri tunakesha hadi saa 9 usiku
kupanga mambo ya kitaifa na Rais Dr Kikwete anaongoza .... Ila sasa hivi
tunataka kupeleka Rais tia maji tia maji wa kupeleka Rais anayeweza
kukesha na kuongea dakika tatu... tuache kulifanyia mdhaha Taifa"
Akimnadi
Mwakalebela alisema kuwa wakati wana Iringa wanafurahia kutatuliwa Kero
Yao ya kuuza mawazi baada ya kampeni ya Asas Dairies Ltd kuwekeza
katika kiwanda Cha maziwa ila Mchungaji msigwa anasimama jukwaani kutaka
watanzania kususia bidhaa zake kwa kuwa yupo Ccm .
Alisema
wakati Mchungaji Msigwa na genge linalimpeleka Rais mpiga dili dawa Yao
ni kutoswa Mwezi wa 10 kwa kumchagua Mbunge Mwakalebela ,Rais Dr
Magufuli na madiwani wa CCM Kuchana na wale wanaotaka kutekelezwa
matakwa Yao binafsi .
"Mimi
nataka kuwaambia genge la wapiga dili kuwa hatuwezi kuiachia nchi hii
kwa wapiga dili hadi sasa kwa mwonekano wa CCM kushinda unaonekana
kuwapa kura Ukawa ni kujeruhi nafsi zao bure baada ya matokeo ya wazee
waliohama CCM ndipo watatambua kuwa CCM ni ile ile .... DR Magufuli na
Mwakalebela pamoja na madiwani watashinda tu"
Hivyo alisema kuwa wakimchagua Mwakalebela kwa kila jambo la Iringa atahakikisha anashirikiana kulipigania kwa nguvu zote .
Kwa
upande wake Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa Hassan Mtenga alisema chama
kimejipanga kuzunguka kata zote kusoma bajeti ya mfuko wa jimbo ambayo
wananchi wametapeliwa na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo .
Bw
Mtenga alisema kuwa hadi sasa ana faili la kila kata na kiasi cha Pesa
za mfuko wa jimbo ambazo zingepaswa kupelekwa ila hakuna jipya hadi sasa
na kumtaka mbunge huyo kuonyesha alikopeleka Pesa za wananchi.
Hata
hivyo alimtaka Mchungaji Msigwa kusimama jukwaani kuwaeleza wananchi
wake kwa miaka mitano kazi gani ya kimaendeleo ameifanya jimbo la Iringa
Mjini zaidi ya kufanya maandamano na kupelekea vijana kufungwa.
Akiomba
kura kwa wananchi hao Mgombea Ubunge jimbo la Iringa mjini Bw
Mwakalebela alisema atahakikisha anafanya Kazi na makundi yote bila
kuwabagua na vyama vyote atafanyanao Kazi.
Alisema
kila kata atazunguka na kueleza kipaumbele chake na jinsi gani
atakavyowatumikia wananchi hao wa jimbo la Iringa ambao wamepata
machungu makubwa kwa miaka mitano hivyo kuwataka kuondokana na machungu
hayo kwa kuchagua CCM
0 comments:
Post a Comment