Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Kibiki azizungumza na kijana, fundi viatu wa mjini Iringa!
Na mwandishi wetu, Iringa
VIJANA wa
stendi kuu ya mabasi ya mjini Iringa, wameanzisha timu ya mpira wa miguu ya ‘Kibiki
Football Club’ili kuunga mkono harakati za mwanahabari wa gazeti la Uhuru na
mzalendo, baada ya kutangaza nia kuwania jimbo hilo.
Katibu wa
timu hiyo, Charles Manet alisema wameamua kuanzisha timu ya mpira wa miguu
inayoitwa Kibiki, ili kuonyesha dhamira yao ya dhati katika kumsaidia kijana
mwenzao.
“Yeye
mwenyewe hakujua kama tumetumia jina lake kwenye timu yetu, tayari tumeshacheza
mechi mbili tangu timu yetu ianze kuitwa Kibiki FC na tunatarajia kuendelea
kucheza mechi za kirafiki, tukianza na timu ya Wambi ya stendi kuu ya mjini
Mafinga,”alisema
Maneti
alisema wamekuwa wakisafiri kwa kuchangishana fedha na kwamba tayari wamepata
jezi seti moja, kutoka kwa wadau mbali mbali wa michezo mjini Iringa.
Aliwataka
wapenzi wa soka la mjini Iringa kuunga mkono jitihada za vijana hao katika
kuhakikisha, timu hiyo inasonga mbele badala ya kuikatisha tama.
“Pamoja na
kukatishwa tama tangu tuunde timu hii lakini ukweli ni kwamba, hatutaacha kwa
sababu Kibiki ni kiongozi na tusipomuunga mkono kijana mwenzetu tutakuwa
hatujamtendea haki hata kidogo,”alifafanua.
Kabla ya
kuunda timu hiyo vijana hao, walichangishana fedha zaidi y ash laki moja na
kumkabidhi Kibiki, wakimtaka azitunze kwa ajili ya kuchukulia fomu ya kuwania
nafasi ya Ubunge katika jimbo la Iringa, muda ukifika.
Wakizungumzia
ubunge, vijana hao walisema kuwa jamii ya wana Iringa inatarajia kumpata kiongozi
anayetokana na wenyewe, kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) ili wampigie kura ya
kuwa mbunge wa jimbo hilo na sio vinginevyo.
Tangu
alipotangaza nia ya kuwania jimbo hilo, Kibiki amekuwa akikubaliwa na makundi
mbalimbali wakiwemo vijana, walemavu, wanawake na wazee.
0 comments:
Post a Comment