Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
|
Katibu wa UVCCM Taifa Bw Sixtus Mapunda mwenye kofia ya ccm akishiriki mchezo wa kimasai leo wakati wa uzinduzi wa tawi la CCM eneo la wafugaji kijiji cha Idodi |
|
mjumbe wa baraza kuu la utekelezaji la UVCCM Taifa Secky Kasuga kulia akishiriki na viongozi wa kitaifa kucheza ngoma ya kimasai |
|
viongozi wa kitaifa wa UVCCM Taifa wakishiriki kucheza na masai |
|
Wananchi wakiwa juu ya miti wakimsikiliza katibu mkuu wa UVCCM taifa leo kijiji cha Idodi |
|
wananchi wa Idodi wakiwa katika mkutano wa katibu wa UVCCM Taifa |
|
katibu wa UVCCM taifa kulia akimpongeza kada wa CCM |
|
Masai wakiwa cheza ngoma |
|
katibu mkuu wa UVCCM Taifa Sixtus Mapunda akisimikwa kwa mlezi wa tawi la Uvccm kulia ni Bi Secky Kasuga |
|
kada wa CCM Bi Juliana Shonza akicheza ngoma ya kimasai leo Idodi |
|
katibu mkuu UVCCM Bw Sixtus Mapunda akimpokea kada wa Chadema Idodi aliyejiunga na CCM leo |
|
Mkuu wa shule ya sekondari Idodi akitoa taarifa ya kuungua kwa mabweni ya wanafunzi |
|
Kada wa Chadema akivishwa kofia ya CCM na katibu mkuu wa UVCCM Taifa Bw Mapunda leo |
|
diwani wa Idodi Bw Onesmo Mtatifikolo akijibu maswali ya wananchi leo |
|
Bweni la sekondari ya Idodi ambalo mbunge wa jimbo la Ismani wiliam Lukuvi na wadau mbali mbali wamelikarabati baada ya kuungua moto |
|
katibu mkuu wa UVCCM Taifa Bw Sixtus Mapunda akiwahutubia wananchi wa Idodi jimbo la Isimani leo |
|
katibu mkuu wa UVCCM Taifa akifurahi jambo na katibu tarafa ya Idodi leo |
|
viongozi wa CCM wilaya ya Iringa ,mkoa na taifa wakiungana na katibu mkuu wa UVCCM Taifa kufanya sala katika makaburi ya wanafunzi 12 walioteketea kwa moto shule ya sekondari Idodi mwaka juzi |
|
mkuu wa shule ya sekondari Idodi akimkabidhi taarifa ya shule katibu mkuu wa UVCCM Taifa Bw Mapunda leo |
|
Mratibu wa wana CCM wa vuyuo vikuu Bw Ramadhan Baraza kulia akiwa katika kibao chenye majina ya wanafunzi waliokufa moto Idodi sekondari |
|
katibu mkuu wa UVCCM taifa akiwa na viongozi wengine kwenye kibao chenye majina ya wanafunzi waliokufa kwa moto Idodi sekondari mwaka juzi |
|
Katibu wa UVCCM mkoa wa Iringa E. Mwampashi akimtambulisha Juliana Shonza |
|
Walimu Idodi wakiwa katika kikao na katibu mkuu wa UVCCM leo |
|
Mkuu wa shule ya sekondari Idodi Bw Cristopher Mwasomola akitoa taarifa ya shule hiyo |
|
katibu mkuu akikagua jengo la bweni lililoungua moto Idodi sekondari |
|
Hili ndilo bweni lililowaka moto |
|
Katibu mkuu UVCCM taifa akimsikiliza mkuu wa shule ya sekondari Idodi leo |
|
Wananchi Idodi wakimsikiliza katibu mkuu wa UVCCM Taifa |
|
katibu mkuu UVCCM Bw Mapunda akikabidhi kadi kwa wanachama wapya wa CCM Idodi |
|
katibu mkuu UVCCM akiongoza wanachama wapya wa CCM kula kiapo |
|
Secky Kasuga akifuatilia hotuba ya katibu mkuu |
|
Bw Mapunda akizungumza na walimu wa shule ya sekondari Idodi leo |
Na matukiodaimaBlog
KATIBU
mkuu wa jumuiya ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi
(UVCCM) Taifa Bw Sixtus Mapunda amempongeza mbunge wa jimbo la
Isimani Bw Wiliam Lukuvi kwa kuwa mbunge wa mfano katika jimbo
lake na kuwa waziri wa mfano katika baraza la mawaziri kutokana
na utendaji kazi wake mzuri unaorejesha heshima ya CCM kwa wananchi
hasa katika kumaliza kero ya ardhi hapa nchini.
Mbali
ya pongezi hiyo Mapunda ameeleza kufurahishwa na mchango wa mbunge
Lukuvi wa bati 503 ,Saruji mifuko 200 na pesa kiasi cha Tsh
milioni 10 kwa ajili ya kusaidia ukarabati wa bweni la wanafunzi
wa shule ya sekondari Idodi lililoungua na moto kutokana na hitirafu
ya umeme hivi karibuni.
Bw
Mapunda ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wananchi wa
kijiji cha Idodi jimbo la Ismani wakati wa ziara yake ya kichama
katika jimbo hilo kwa ajili ya kuhamasisha wananchi kujitokeza
kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.
Alisema
kuwa hakuna sababu ya wananchi wa Isimani kuhangaika na mbunge
zaidi ya Lukuvi kutoka na kazi kubwa ya kimaendeleo ambayo mbunge
huyo ameifanya ndani ya jimbo hilo na kuwa hadi sasa hakuna mbunge
ambae upepo wa kisiasa kwa wananchi wake ni mzuri kama ilivyo kwa
mbunge Lukuvi .
Kwani
alisema pamoja na Lukuvi ambae ni waziri wa ardhi kuleta
maendeleo katika jimbo lake bado amekuwa ni waziri mchapakazi
kwa kufanya kazi kwa vitendo zaidi kwa kuwasaidia wananchi wenye
kero mbali mbali za ardhi kupata haki yao .
"Nawaombeni
kama kuna mpinzani wa Chadema anakuja kutaka ubunge Isimani
muulizeni anataka kuwafanyia nini cha kimaendeleo na amefanya nini
ikiwa hata saruji mfuko mmoja sekondari ya Idodi ameshindwa
kupeleka ......nawaombeni sana msimpoteze Lukuvi ni mbunge mchapa
kazi" alisema
katika
kuunga mkono jitihada za mbunge Lukuvi na jitihada za wadau mbali
mbali ambao wamejitokeza kuchangia maafa katika shule ya
sekondari Idodi kwa upande wake anawaagiza vijana wote wa UVCCM
mkoa wa Iringa kuandaa kambi ya kufyatua tofari za kujengea bweni
mmoja katika shule hiyo ya sekondari Idodi kuanzia mwezi ujao
ili kuwezesha wanafunzi kupata bweni la kuishi .
Mapunda
alisema kuwa kwa upande wake atasaidia bati 770 kwa ajili ya
ujenzi wa bweni hilo na kuwataka wananchi kujenga utamaduni wa
kuendelea kushiriki shughuli za kimaendeleo na kuchagua CCM ambao
wanatenda kwa vitendo badala ya wapinzani ambao wao kazi yao ni
kufanya maandamano na sio maendeleo .
Kuhusu
suala la majanga ya moto katika shule ya sekondari Idodi
aliuagiza uongozi wa shule hiyo pamoja na serikali ya wilaya kwa
kushirikiana na shirika la umeme Taifa Tanesco kufanya uchunguzi wa
kina ili kujua chanzo cha moto wa mara kwa mara shuleni hapo na
kuwa yawezekana chanzo si mfumo wa uunganishaji wa umeme katika
bweni ila upo kwa Tanesco wenyewe kwa umeme kuzidi na kupungua .
katika
ziara yake hiyo pia katibu huyo na msafara wake walipata
kutembelea makaburi ya wanafunzi 12 walioteketea kwa moto katika
shule ya sdekondari Idodi na kufanya sala fupi ya kuwakumbuka
wanafunzi hao ambao hadi sasa majina yao wote yamepatikana baada
ya vipimo vya DNA kurudi kutokana na awali kuzikwa bila
kutambuliwa na kuona jinsi ambavyo serikali ilivyoboresha eneo
hilo kwa kuweka uzio ili kuwaondoa hofu wanafunzi wengine.
Katika
risala yake kwa katibu mkuu huyo mkuu wa shule ya sekondari
Idodi Bw Christopher Mwasomola alisema kuwa mbunge wa jimbo hilo
Bw Lukuvi ndie aliyekuwa mtu wa kwanza kusaidia ukarabati wa
mabweni yaliyoungua moto kwa kutoa Saruji mifuko 200, bati 503
,madogoro 100 na fedha kiasi cha Tsh milioni 10 na kuwa bila
jitihada hizo za mbunge wao yawezekana hadi sasa ukarabati huo
usingefanyika .
Aliwataja
wadau wengine waliofika kusaidia kuwa ni pamoja na Ruaha
Carnivores Project waliotoka madogoro 48, Paroko Salvatory Tsh
milioni 1, Askofu wa kanisa la RC jimbo la Iringa Tsh milioni 1 na
sabuni kwa wanafunzi wote , TOHASSA Iringa Tsh 900,000, Shule mbali
mbali za sekondari zilichangia vitu mbali mbali zikiwemo kalamu
,sabuni na vifaa vingine , Shule ya msingi Idodi Tsh 100,000,
Balozi wa Dubai Tsh 9,927,000 na mbunge wa viti maalum mkoa wa
Iringa Bi Chiku Abwao(Chadema) Tsh milioni 1
Hata
hivyo alisema changamoto kubwa ni kukosekana kwa bweni la
wasichana shuleni hapo na kupelekea wanafunzi kwa sasa kulala
jengo la mazingira ukumbi wa mikutano pia kukosekana kwa utulivu
kwa wanafunzi shuleni hapo .
Mkuu
huyo pia alimpongeza katibu mkuu huyo wa vijana kwa kuwa
kiongozi wa mfano katika jamii na kuwa alichokifanya katika shuleni
hiyo ndicho ambacho wananchi wanapenda na sio maneno bila
vitendo .
0 comments:
Post a Comment