Home » » KATIBU MKUU WA UVCCM TAIFA ASIFU UTENDAJI KAZI WA WAZIRI LUKUVI JIMBONI NA WIZARANI ATOA AGIZO KWA VIJANA KUSAIDIA UJENZI WA BWENI IDODI SEKONDARI.‏

KATIBU MKUU WA UVCCM TAIFA ASIFU UTENDAJI KAZI WA WAZIRI LUKUVI JIMBONI NA WIZARANI ATOA AGIZO KWA VIJANA KUSAIDIA UJENZI WA BWENI IDODI SEKONDARI.‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Katibu wa  UVCCM Taifa  Bw Sixtus  Mapunda  mwenye  kofia ya ccm  akishiriki   mchezo wa   kimasai  leo  wakati  wa uzinduzi  wa tawi la  CCM eneo  la  wafugaji kijiji  cha  Idodi 
mjumbe  wa  baraza  kuu la  utekelezaji  la UVCCM Taifa  Secky Kasuga kulia akishiriki na  viongozi  wa  kitaifa  kucheza ngoma ya  kimasai
viongozi  wa  kitaifa  wa UVCCM Taifa  wakishiriki kucheza na masai
Wananchi  wakiwa  juu ya  miti  wakimsikiliza katibu  mkuu wa UVCCM taifa  leo kijiji cha Idodi
wananchi  wa  Idodi  wakiwa katika mkutano wa katibu  wa UVCCM Taifa
katibu  wa UVCCM taifa  kulia akimpongeza kada wa CCM
Masai  wakiwa cheza  ngoma
katibu  mkuu  wa  UVCCM Taifa Sixtus Mapunda  akisimikwa  kwa  mlezi  wa tawi la Uvccm kulia ni Bi Secky Kasuga
kada  wa CCM Bi Juliana Shonza  akicheza  ngoma  ya  kimasai  leo Idodi
katibu  mkuu  UVCCM Bw Sixtus Mapunda  akimpokea  kada  wa Chadema  Idodi aliyejiunga na  CCM leo
Mkuu  wa  shule ya  sekondari  Idodi  akitoa taarifa ya kuungua kwa mabweni ya  wanafunzi 
Kada  wa Chadema  akivishwa kofia ya  CCM na katibu  mkuu wa UVCCM Taifa  Bw Mapunda leo
diwani  wa Idodi  Bw  Onesmo Mtatifikolo akijibu maswali ya  wananchi  leo
Bweni la sekondari ya  Idodi  ambalo mbunge  wa  jimbo   la Ismani wiliam Lukuvi na  wadau  mbali mbali  wamelikarabati  baada ya  kuungua  moto
katibu  mkuu  wa UVCCM Taifa  Bw Sixtus Mapunda  akiwahutubia  wananchi  wa Idodi  jimbo la Isimani  leo
katibu  mkuu  wa UVCCM Taifa  akifurahi jambo na katibu tarafa ya  Idodi  leo
viongozi  wa CCM wilaya  ya  Iringa ,mkoa na  taifa  wakiungana na katibu  mkuu wa UVCCM Taifa  kufanya  sala katika makaburi ya  wanafunzi 12  walioteketea kwa  moto  shule ya  sekondari  Idodi  mwaka  juzi
mkuu  wa  shule ya sekondari  Idodi  akimkabidhi taarifa ya  shule katibu mkuu  wa UVCCM Taifa  Bw Mapunda  leo
Mratibu  wa  wana CCM  wa  vuyuo  vikuu Bw  Ramadhan  Baraza   kulia akiwa katika  kibao  chenye majina ya wanafunzi  waliokufa  moto Idodi  sekondari
katibu  mkuu  wa UVCCM taifa  akiwa  na  viongozi wengine  kwenye  kibao  chenye majina  ya  wanafunzi  waliokufa kwa  moto  Idodi  sekondari  mwaka  juzi
Katibu  wa UVCCM mkoa  wa  Iringa E. Mwampashi akimtambulisha  Juliana Shonza
Walimu  Idodi wakiwa katika  kikao na  katibu  mkuu wa UVCCM leo
Mkuu  wa  shule  ya  sekondari  Idodi  Bw  Cristopher Mwasomola  akitoa  taarifa ya  shule  hiyo
katibu mkuu  akikagua  jengo  la  bweni  lililoungua  moto   Idodi  sekondari
Hili  ndilo  bweni  lililowaka  moto 
Katibu  mkuu  UVCCM taifa  akimsikiliza  mkuu  wa  shule ya  sekondari Idodi  leo
Wananchi  Idodi  wakimsikiliza katibu mkuu  wa  UVCCM Taifa
katibu  mkuu  UVCCM Bw  Mapunda  akikabidhi kadi kwa wanachama  wapya wa CCM Idodi
 katibu mkuu  UVCCM akiongoza wanachama  wapya  wa CCM kula  kiapo
Secky Kasuga  akifuatilia  hotuba ya  katibu mkuu
Bw  Mapunda  akizungumza na  walimu  wa shule ya sekondari  Idodi  leo
Na matukiodaimaBlog

KATIBU  mkuu  wa   jumuiya ya  umoja  wa  vijana  wa  chama  cha mapinduzi (UVCCM) Taifa  Bw  Sixtus  Mapunda amempongeza  mbunge  wa  jimbo la Isimani Bw  Wiliam Lukuvi kwa  kuwa  mbunge  wa  mfano katika  jimbo  lake na kuwa  waziri  wa  mfano  katika  baraza la  mawaziri kutokana na  utendaji kazi  wake  mzuri unaorejesha heshima  ya CCM kwa  wananchi hasa katika  kumaliza kero ya ardhi  hapa  nchini.

Mbali ya  pongezi  hiyo Mapunda ameeleza  kufurahishwa na mchango  wa mbunge  Lukuvi  wa bati 503 ,Saruji  mifuko 200  na  pesa  kiasi cha Tsh milioni 10  kwa ajili ya  kusaidia  ukarabati  wa  bweni la  wanafunzi  wa  shule ya  sekondari Idodi  lililoungua na moto  kutokana na hitirafu ya  umeme  hivi karibuni.

Bw  Mapunda  ameyasema  hayo  leo  wakati  akizungumza na wananchi  wa kijiji cha Idodi  jimbo la Ismani  wakati  wa  ziara  yake ya kichama katika jimbo    hilo kwa  ajili ya  kuhamasisha  wananchi  kujitokeza kwa wingi kujiandikisha  katika  daftari la  kudumu la  wapiga  kura.

Alisema  kuwa hakuna  sababu ya  wananchi  wa Isimani  kuhangaika na  mbunge  zaidi  ya  Lukuvi  kutoka na kazi kubwa ya  kimaendeleo ambayo  mbunge   huyo  ameifanya  ndani ya jimbo  hilo na  kuwa hadi  sasa hakuna mbunge ambae upepo  wa  kisiasa kwa wananchi wake ni mzuri kama  ilivyo kwa  mbunge  Lukuvi .

Kwani  alisema  pamoja na  Lukuvi ambae ni  waziri  wa ardhi  kuleta  maendeleo  katika  jimbo lake  bado  amekuwa ni  waziri  mchapakazi  kwa  kufanya kazi kwa  vitendo  zaidi  kwa  kuwasaidia  wananchi  wenye  kero mbali mbali  za ardhi  kupata  haki  yao .

"Nawaombeni  kama  kuna  mpinzani wa Chadema anakuja  kutaka  ubunge  Isimani muulizeni anataka  kuwafanyia  nini  cha  kimaendeleo  na amefanya  nini ikiwa hata  saruji  mfuko  mmoja sekondari ya  Idodi ameshindwa  kupeleka  ......nawaombeni sana msimpoteze  Lukuvi ni   mbunge mchapa  kazi" alisema

katika  kuunga  mkono  jitihada  za mbunge  Lukuvi na  jitihada za  wadau mbali mbali ambao  wamejitokeza  kuchangia  maafa katika  shule  ya sekondari  Idodi kwa upande  wake anawaagiza  vijana wote  wa UVCCM mkoa  wa  Iringa kuandaa kambi ya kufyatua  tofari za  kujengea bweni mmoja  katika  shule   hiyo ya sekondari  Idodi   kuanzia  mwezi  ujao  ili  kuwezesha  wanafunzi kupata  bweni la  kuishi .

Mapunda  alisema  kuwa  kwa upande  wake  atasaidia bati  770  kwa  ajili ya ujenzi  wa  bweni   hilo na  kuwataka  wananchi  kujenga  utamaduni wa  kuendelea  kushiriki  shughuli za kimaendeleo na  kuchagua CCM ambao  wanatenda kwa  vitendo  badala ya  wapinzani  ambao wao kazi yao ni kufanya maandamano  na  sio  maendeleo .

Kuhusu  suala la  majanga  ya  moto  katika  shule ya  sekondari  Idodi  aliuagiza  uongozi  wa shule  hiyo  pamoja na  serikali ya  wilaya  kwa  kushirikiana na shirika la umeme  Taifa Tanesco  kufanya uchunguzi  wa  kina  ili  kujua  chanzo  cha moto wa  mara kwa mara  shuleni hapo  na  kuwa  yawezekana  chanzo  si mfumo  wa  uunganishaji wa umeme katika  bweni ila  upo   kwa Tanesco  wenyewe kwa  umeme  kuzidi na  kupungua .

katika   ziara   yake hiyo  pia katibu  huyo na msafara  wake  walipata  kutembelea  makaburi  ya  wanafunzi  12  walioteketea kwa moto  katika  shule  ya  sdekondari  Idodi  na  kufanya  sala  fupi ya  kuwakumbuka wanafunzi hao ambao  hadi  sasa majina  yao wote yamepatikana  baada  ya  vipimo  vya  DNA kurudi kutokana  na  awali  kuzikwa bila  kutambuliwa na  kuona  jinsi  ambavyo   serikali  ilivyoboresha  eneo  hilo kwa kuweka  uzio  ili  kuwaondoa hofu  wanafunzi wengine.

Katika  risala  yake  kwa  katibu  mkuu  huyo mkuu  wa shule ya  sekondari  Idodi  Bw  Christopher Mwasomola alisema  kuwa  mbunge  wa  jimbo  hilo Bw  Lukuvi ndie  aliyekuwa mtu wa  kwanza kusaidia ukarabati  wa mabweni  yaliyoungua moto  kwa  kutoa Saruji  mifuko 200, bati 503  ,madogoro 100 na fedha  kiasi  cha Tsh milioni  10  na  kuwa bila jitihada  hizo  za mbunge  wao yawezekana hadi  sasa ukarabati  huo  usingefanyika .

Aliwataja   wadau  wengine  waliofika  kusaidia  kuwa ni pamoja na  Ruaha Carnivores Project waliotoka  madogoro 48, Paroko Salvatory   Tsh  milioni 1, Askofu wa  kanisa la RC jimbo la  Iringa Tsh  milioni 1  na  sabuni kwa  wanafunzi wote , TOHASSA Iringa  Tsh  900,000, Shule  mbali mbali  za  sekondari zilichangia vitu  mbali mbali zikiwemo kalamu ,sabuni  na  vifaa  vingine  , Shule ya msingi Idodi Tsh 100,000, Balozi  wa Dubai  Tsh 9,927,000  na mbunge  wa viti maalum  mkoa  wa Iringa Bi  Chiku  Abwao(Chadema) Tsh milioni 1

Hata   hivyo  alisema  changamoto  kubwa ni  kukosekana kwa  bweni la  wasichana  shuleni  hapo na  kupelekea  wanafunzi kwa  sasa  kulala jengo  la mazingira  ukumbi wa mikutano  pia  kukosekana kwa utulivu kwa  wanafunzi  shuleni hapo .

Mkuu  huyo  pia  alimpongeza  katibu  mkuu  huyo  wa vijana  kwa  kuwa  kiongozi  wa  mfano katika  jamii na  kuwa alichokifanya katika shuleni  hiyo ndicho  ambacho  wananchi  wanapenda  na  sio maneno  bila  vitendo .

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa