Home » » WANANCHI LUILO WAMCHONGEA DIWANI WAO KWA MBUNGE FILIKUNJOMBE WATAKA ACHAPWE FIMBO‏

WANANCHI LUILO WAMCHONGEA DIWANI WAO KWA MBUNGE FILIKUNJOMBE WATAKA ACHAPWE FIMBO‏



mbunge  wa Ludewa Deo Filikunjombe akipongezwa na masisita  wa parokia ya Luilo kwa kuwapigania  kupata  umeme


mbunge Filikunjombe kushoto na diwani  wa  Ludewa  mjini Monica Mchilo wakishirikiaana kushusha saruji mifuko 50 na bati 50 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya songambele
mbunge Filikunjombe kushoto na diwani  wa  Ludewa  mjini Monica Mchilo wakishirikiaana kushusha saruji mifuko 50 na bati 50 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya songambele
mbunge Filikunjombe  akizungumza na wananchi wa kitongoji cha Ngalawale


mbunge Filikunjombe akishuka katika trekita baada ya kusaidia kushusha saruji na bati
mwenyekiti  wa kijiji  cha kipangala akimchongea diwani  huyo kwa  mbunge  juu ya kuzuia kushiriki mqaendeleo
wananchi Luilo wakimpinga  diwani  wao mbele ya  mbunge

mbnge Filikunjombe akiwahutubia wananchi wa Luilo

mkazi  wa Ngalewale
mmoja  kati ya  wazee  wa  mtaa  wa Ngalewala   kushoto akimpongeza  mbunge Filikunjombe kulia huku  akimtaka achukue fomu wao wanampenda aendelee  kuwa mbunge wao
Diwani  Matei Kongo

    Na matukiodaimablog

WANANCHI wa  kijiji  cha Luilo kata ya Luilo  wilaya ya  Ludewa  mkoani  Njombe  wamemkataa mbele  ya  mbunge  Deo  Filikunjobe ,diwani  wao  wa kata ya  Luilo  Matei kongo (CCM) ambae ni mwenyekiti  wa Halmashauri ya  Ludewa  na kutaka acharazwa  bakora hadharani kutokana na kuwa  mpinzani  wa maendeleo katika kata ya Luilo.

Wananchi hao  walimlalamikia  diwani   huyo  katika  mikutano  ya hadhara wa mbunge Filikunjombe  aliyoifanya  kwenye  vijiji vya Lifua na Luilo kwa  lengo la   kuhamasisha wananchi kushirikiana na  mkandarasi  wa mradi  wa umeme  kati
ka  shughuli za  kuchimba mashimo .
 

Wakizungumza katika  mkutano  huo wananchi hao walisema  kuwa  wanashangazwa na  hartua ya   diwani  wao mbali ya  kuwa ni diwani  wa CCM  ila  ameendelea  kuwa mpinzani  mkubwa wa maendeleo  katika  kata  yake  kwa   kupinga kila shughuli ya maendeleo inayofanywa mbunge  katika kata  yake.

mkazi  wa kijiji  cha  Luilo  Osward  Haule alisema  wakati  serikali ya  CCM ikihimiza wananchi kushiriki  katika  shughuli za kmaendeleo kwa  kujitolea  nguvu  zao  diwani   huyo amekuwa akienda  kinyume  kwa  kuzuia  wananchi kushiriki katika shughuli za  kimaendeleo na  kuwa katika kata   hiyo kuna ujenzi  wa  zahanati unaoendelea kwa  zaidi ya  miaka minne sasa  bila  kukamilika kutokana na ubinafsi  wa  diwani  huyo.

' mbunge wetu umekuwa  ukifanya kazi kubwa  sana  ya  kutuletea maendeleo katika jimbo la Ludewa na  hatujapata    kuwa na mbunge anayejituma  kuleta  maendeleo kama  wewe  toka  nchi  hii  ipate  uhuru  ila kikwazo kikubwa kipo hapa  mbele kwenu  viongozi  kwani diwan wetu kweli  tunashindwa  kumuelewa na mpinzani ama  ni diwani  wa ccm kila jema   linalofanywa na  mbunge yeye kazi  yake ni  kupinga ......sasa inapendezwa  sana wapinga maendeleo wakati  mwingine kuonywa kwa viboko'

Alisema   kuwa sababu  kubwa ya kata   hiyo kukwama  baadhi ya miradi  ya  kimaendeleo ni  kutokana na  diwani wao kuwa kibinafsi  zaidi na  kuonyesha   wazi  wazi upinzani wa kazi zinazofanmywa na mbunge  hivyo kwa  upande  wao wanamtaka diwani   huyo  kukaa pembeni  ili  wao wateue diwani  wao  wa  muda atakayeshirikiana na  mbunge kuwaletea maendeleo kwa  muda  uliobaki na baada ya hapo  muda  wa  uchaguzi ukifika  wamchague diwani  wa  wananchi nje ya diwani  huyo.

kwani  alisema  wao  kama  wananchi  wapo tayari  kwenda  kushiriki  maendeleo  ila  shida  ipo  kwa  diwani ambae  amekuwa  akiwazuia kushiriki shughuli za kimaendeleo hasa  katika  miradi  inayoanzishwa na  mbunge .

Hata  hivyo  alisema kwenye  kijiji   hicho  kuna mradi wa  ujenzi  wa  zahanati  ambao umeendelea kukwama kwa zaidi ya  miaka  minne  sasa  huku kazi kubwa ya diwani  wao ni kujitolea gari la kusafirisha maiti kutoka Halmashauri  pindi  wananchi  wa kata hiyo  wanapopatwa na msiba  badla ya kusimamia ujenzi  wzahanati hiyo ili  kupunguza vifo.

mwenyekiti  wa kijiji  cha kipangala Jeremia kayombo alimweleza  mbunge  huyo  katika mkutano  kuwa  diwani  huyo  alimpigia  simu siku moja  baada ya mbunge kupita  kuhamasisha  wananchi kushiriki shughuli za uchimbaji mashimo ya  nguzo za  umeme akimtaka  azuie wananchi wasishiriki maendeleo japo viongozi na wananchi  walimpuuza.

'mimi kama  mwenyekiti  wa kipangala ninae  tokana na ccm sipotayari  kusema uongo hapa  nitasema kweli tupu kama chama  chetu  ccm kinavyotaka huyo  diwani ni mpinzani mkubwa wa maendeleo alinipigia simu kutaka nizuie  wananchi kushiriki katika maendeleo'

Alisema  hata  sababu ya  kutoshiriki  katika  mikutano  hiyo ya  mbunge kwa  diwani  huyo ni  kutokana na kukwepa hasira  za  wananchi dhidi  yake  japo mara kwa mara mbunge anapofanya ziara katika kata yake  huwa anatoa sababu mbali mbali za  kutoshiriki .

Akiwahutubia  wananchi hao mbunge  Filikunjombe mbali ya  kuwapongeza  kwa  hatua  waliyoichukua ya kumpuuza diwani  huyo bado  alisema kwa  upande  wake kama mbunge hatapenda kuona  wananchi wakikosa maendeleo kutokana na vikwazo  vya  kiongozi mmoja na  kuwa kwa nguvu  zake na ushirikiano  wa wananchi wa kata   hiyo lazima umeme  ufike.

Filikunjombe  alisema yupo tayari kugombana na  mtu  mmoja anayekwamisha  maendeleo  na mara baada ya umeme  kuwaka  atapatana  ila  si vinginevyo  kwani  wanaopata  shida ni wananchi na sio viongozi .
Alisema  kuwa ni  kweli serikali  imetoa pesa  kwa mkandarasi  kwa  ajili ya  umeme ila kwa kasi ya mkandarasi  uwezekano  wa  umeme   huo  kukamilika mwaka   huu ni  ndoto kutokana na kasi  ndogo na mkandarasi  aliyepewa kazi hiyo ni  mmoja kwa  mkoa mzima  wa Njombe hivyo kwa  upande wake kwa  kutumia mbinu  zake amefanikiwa  kupata nguvu na  kutaka umeme   huo kuwaka baada ya  miezi miwili kwa vijiji vyote  zaidi ya 12 vya jimbo la Ludewa .

Mbunge  huyo  alisema  kuwa baadhi ya maeneo umeme  umekuwa  ukichelewa  kufika kutokana na wananchi kuleta  vikwazo vya  kudai fidia ya miti na mazao  ila kwa  wilaya ya  Ludewa amefanikiwa  kuwaomba  wananchi  wasidai fidia ya miti na  wao  wenyewe  kushiriki kuchimba mashimo na  wamekubali  katika kata zote na madiwani  wanashiriki vizuri katika maendeleo  ila shida ni kwa diwani  huyo wa Luilo .

kuwa gharama  ya  uchimbaji shimo moja ni Tsh 5000 na  kuwa jumla  ya mashimo kama 15   hivyo ni kiasi  cha sh 75,000 ambazo kama  kulipwa  wananchi hao  wangelipwa na ukigawa kwa  kila mwananchi  ni kama sh 150 na kama kazi   hiyo ya uchimbaji ingefanywa na mkandarasi kwa mafundi wake ingechukua muda  mrefu zaidi hivyo ndio  sababu ya kuwaomba wananchi kujitolea  nguvu zao.

Pia  alisema kwa  upande wake kwa ajili ya kuwaunga  mkono atawasaidia kukamilisha zahanati  hiyo ili  kuepukana na shida  ya zahanati

 Akizungumza kwa  njia ya simu  kuhusiana na malalamiko ya wananchi  wake diwani Kongo alikiri kuwazuia  wananchi  kushiriki katika maendeleo ya mradi  huo  wa umeme huku akidai kuwa  yeye ni mwenyekiti wa halmashauri ya  Ludewa .

Kongo  alisema  kwa  kuwa mkandarasi kapatikana hata kama wananchi  watapata  umeme kwa kuchelewa  ni sawa tu .

mkandarasi  wa  mradi  huo wa  umeme Bw Aron  Makulu alisema alisema  kuwa kampuni  yake uwezo haina  uwezo  wa  kuwalipa wananchi pesa ila fedha  zilizopo za  kulipa wafanyakazi pekee.


katibu mwenezi  wa ccm mkoa  wa Njombe Honoratus Mgaya  alisema  kuwa chama  cha mapinduzi ni chama  kizuri  sana  kinachowajali  wananchi wake  ila shida ni baadhi ya viongozi ndio  wanaokichafua chama na kuwafanya  wananchi  wakione  chama kibaya na  kuwa kama chama hakitakubali kuchukiwa na  wananchi kwa ajili ya mtu  mmoja na  kuwataka  wananchi  hao kuwapuuza viongozi wasiopenda maendeleo.


Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa