Home » » MBUNGE GODFREY MGIMWA AUNGA MKONO UANZISHWAJI WA VICOBA VIJIJI VYOTE VYA KATA YA WASA ,ACHANGIA MILIONI 2.4 ,ASEMA UBUNGE BADO ANAUTAMANI‏

MBUNGE GODFREY MGIMWA AUNGA MKONO UANZISHWAJI WA VICOBA VIJIJI VYOTE VYA KATA YA WASA ,ACHANGIA MILIONI 2.4 ,ASEMA UBUNGE BADO ANAUTAMANI‏


Mbunge wa jimbo la Kalenga Bw  Godfrey Mgimwa

Wananchi  wanachama wa VICOBA  kata ya  Wassa  wakiwa katika uzinduzi wa VICOBA
Wanachama wa VICOBA kata ya  wasa wakiwa katika hadfla ya uzinduzi
Mbunge wa  jimbo la kalenga Bw  Mgimwa wa  pili  kulia akiteta jambo
katibu  wa mbunge wa Kalenga Bw Martine  Simangwa kulia na mbunge wa jimbo la Kalenga Bw Mgimwa wakiwa katika  uzinduzi wa VICOBA kata ya  wasa
Wananchi  wa kata ya Wasa wakiwa katika  uzinduzi wa Vicoba
 Na MatukiodaimaBLog
KATIKA  harakati  za  kuwakomboa  wananchi  wa  jimbo la Kalenga  kiuchumi mbunge  wa  jimbo la Kalenga  wilayani  Iringa Bw  Godfrey Mgimwa amechangia  kiasi cha Tsh milioni 2.4 kwa  ajili ya  kuunga mkono  jitihada za  wapiga  kura  wake wa  vijijini vya 6  vya  kata ya   wasa.

Pamoja na  kuchangia  kiasi  hicho cha  fedha  mbunge  Mgimwa amewahakikishia  wananchi  hao wa kata ya  Wasa na  jimbo  zima la  Kalenga  kuwa atagombea  tena  ubunge katika   jimbo  hilo  na  kuwataka  kutosikiliza propaganda zinazoenezwa na baadhi ya  watu  wanaotaka ubunge jimbo  hilo .

Akizungumza na  wananchi  wa  kata ya   Wasa wakati  wa uzinduzi  wa  VICOBA katika  kata   hiyo mbunge  Mgimwa alisema  kuwa wapo  baadhi ya   watu  wamekuwa  wakizunguka katika  jimbo  hilo na  kuwadanganya  wananchi  kuwa  wanataka  kuungwa mkono katika nafasi ya  ubunge  kwa madai kuwa mbunge wa  sasa hawezi  tena  kugombea jambo ambalo ni sawa na upotoshaji na  wananchi  wanapaswa  kuwaogopa  watu hao kama ugonjwa wa ukoma.

"Mimi ndio  mbunge wa  jimbo la Kalenga ambae hadi  sasa ikifika  mwezi wa nne  nitakuwa  nimemaliza mwaka  mmoja  baada ya  kupokea nafasi  hii kwa aliyekuwa  mbunge wa Kalenga Dr  Wiliam Mgimwa ambae alitangulia  mbele  za haki ......hivyo  mimi  leo nawatangazia  rasmi  kuwa ubunge bado nautamani na  nitagombea  tena nafasi ya  ubunge ili  niweze  kuwatumikia  kipindi  cha miaka mitano kamili  na ndipo  mpate kunipima kama kwa kipindi changu kamili  cha miaka  mitano "

Mbunge  Mgimwa alisema  kuwa  jitihada  kubwa amekuwa akizielekeza katika  jimbo  hilo la Kalenga  lengo ni  kuwawezesha  wananchi wake  kutambua utendaji kazi  wake na hata  kutoendelea  kuligeuza jimbo  hilo  kuwa ni  jimbo la watu  kujifunzia  ubunge na  kuwa wakati umefika  kwa wanakalenga kupima  utendaji kazi  wake kwa  kipindi kifupi  cha mwaka mmoja ambacho amepata  kuwaongoza kama mbunge wao.

Alisema  kuwa amefanikiwa kutekeleza ahadi mbali mbali zilizoachwa na mbunge aliyefariki  dunia na  kuwa hadi  sasa ahadi ambazo zimebaki ni chache zaidi na kuwa kabla ya uchaguzi  mkuu Octoba  ahadi  zote  zilizoahidiwa na  mbunge aliyepita  atakuwa amezimaliza na  kuweka  historia ya aina yake kwa  jimbo la Kalenga kwa  kuingia katika uchaguzi  bila  kiporo  cha ahadi.

"Nawaombeni  sana  wananchi  msiogope  kupokea  pesa kwa  wanaojipitisha  kujitangaza kutaka ubunge jimbo la kalenga ila msimamo wenu   uwe ni ule ule wa kutaka  mbunge wa kuwaletea maendeleo  sio mbunge wa  kuwanunua  kwa  fedha na baada ya  kuingia madarakani  kutumia  muda  wake   kurudisha  pesa alizowapa wakati wa  kutaka  ubunge .....wana kalenga wa leo  sio wa mwaka 47 sasa wengi wanataka  kuona kalenga  inasonga mbele na  sio kuendelea  kugeuzwa ni sehemu ya  kujaribu ubunge"

Akizungumzia  juu ya  kuwevizesha  vikundi  hivyo  vya VICOBA alisema  kuwa  lengo ni kuona  Kalenga  inakuwa na banki ya  wananchi wa Kalenga ambayo itasaidia  kuondoa  changamoto mbali mbali zikiwemo  za  pembejeo na  mikopo kwa  vijana ,wazee na  wanawake katika  jimbo hilo ambalo kwa  sasa halina  benki yake .

Alivitaja  vijiji ambavyo  ameviwezesha  kuanzisha VICOBA   ni  vikundi  12  vya kata  hiyo ya  Wasa ambavyo ni kutoka  kijiji  cha Wasa, Usengelindete, Ufyambe, Ihomasa na Ikungwe na  kuwa vikundi  hivyo  vitasaidia  kuwawezesha  wananchi wa kata  hiyo  kiuchumi.

Kwa upande  wao wanachama  wa  vikundi  hivyo  vya  VICOBA   kata ya  Wasa  mbali ya  kumpongeza  mbunge Mgimwa kwa kuwa mbunge wa  mfano  wa kuwezesha  kata  hiyo kuwa na  vikundi hivyo vya  VICOBA bado  walisema  wao  kamwe  hawatanyumbishwa na watu wanaojipitisha ambao  hawajawafanyia  lolote  zaidi ya  kuendelea  kuwabagua kwa  kuwapa  fedha  viongozi wachache wa CCM kata na vijiji  ili kuwapigia  debe lakini  wanachoamini  wao si  wa kupigiwa   debe bali  wanahitaji mbunge mtendaji kama  mbunge ambae anawajali wananchi  wote bila kuwabagua.

Diwani  wa  viti maalum tarafa ya  Kiponzero Vumilia  Mwenda  aliwataka  wanawanchi wa kata  hiyo ya   Wasa  kushiikamana kuwa  wamoja na kuangalia kiongozi mwenye  sura ya  kuwaletea maendeleo kama  ilivyo kwa mbunge  huyo badala ya  kuendelea  kuangalia uwezekano  wa kubadili  wabunge na matokeo yake ni  jimbo  kuendelea kukosa maendeleo .

Mwenyekiti wa UWT  wilaya ya  Iringa  vijijini  Bi Shakra  Kiwanga alisema kuwa ili  kuweze  kusonga mbele  kimaendeleo  wananchi  wa Kalenga  hawanabudi  kuungana na kuwa kitu

kimoja na kuwa na msimamo  katika  kuchangua badala ya  kubadili  wabunge  na  kuwa  kuanzishwa  kwa Vicoba  hivyo ni ukombozi mkubwa kwao.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa