Kamanda wa uvccm wilaya ya Iringa mjini Frederick Mwakalebela akiwahutubia wananchi ktk uwanja wa mwembetogwa ktk mkutano ulioandaliwa na uvccm Iringa mjini
Wananchi Iringa mjini wakiwa ktk mkutano wa uvccm Iringa mjini
kada wa CCM Bw Ahmed Mbata mwenye miwani akimzuia kijana wa CCM kuendelea kumthibiti kada wa Chadema aliyeanguka chini baada ya kupigwa kwa tuhuma za kutaka kuvuruga mkutano wa UVCCM |
Vijana wa CCM wakisogea kumshambulia kijana aliyetaka kuvuruga mkutano wao |
Wananchi wakimtazama kijana wa Chadema aliyetaka kuvuruga mkutano wa CCM |
Wananchi wakitazama tukio hilo |
Askari polisi akizuia vurugu hivyo |
Mwakalebela kushoto akiwa na katibu wa UVCCM Iringa |
Na MatukiodaimaBlog
KAMANDA wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi
(UVCCM) wilaya ya Iringa mjini Frederick Mwakalebela atuma salam kwa
upinzani jimbo la Iringa
mjini kuwa mwisho wao kuongoza jimbo
hilo ni oktoba mwaka huu hivyo wananchi
wajiandae kwa sherehe za kulipokea jimbo.
Akizungumza leo katika mkutano
wa uvccm Iringa mjini uliofanyika katika uwanja wa Mwembetogwa mjini hapa.
Alisema kuwa ni jambo la kushangaza kuona mbunge wa jimbo la Iringa
mjini mchungaji Peter Msigwa akikodi majeshi (wanasiasa wenzake )nje ya Iringa
mjini ili kusaidia mashambulizi baada
ya kuona hali ya
upepo kwakwe si nzuri .
" naomba kuwahakikishieni kuwa jimbo hili tulikosea mwaka 2010 ila
kwa mwaka huu haturudii kosa lazima jimbo lirudi CCM"
Hivyo alisema kuwa ni ukweli usiopingika kuwa lazima Chadema wajipange
kukabidhi jimbo hilo kwa Ccm na kuwa maandalizi ya kupokea yamekwisha fanyika.
Akielezea kuhusu umuhimu wa vijana kujiandikisha katika daftari la
kudumu la wapiga kura alisema ili Ccm uweze kushinda kuanzia udiwani ,ubunge na
Urais ni lazima wakajitokeza kujiandikisha ktk daftari hilo .
Kwani alisema hakuna ushindi bila ya vijana kujitokeza kujiandikisha na
kuwa iwapo kila mmoja atajiandikisha ushindi wa CCM upo wazi .
Kwa upande wake katibu wa CCM
mkoa wa
Iringa Hassan Mtenga akihutubia
wananchi hao alisema kuwa
mbunge msigwa anapaswa kujiandaa kisaikolojia kwani
CCM imejipanga vema kuona
jimbo hilo linarudi
mikononi mwa CCM kwa mwaka huu .
Alisema kuwa jimbo hilo
CCM kililianzimisha kwa Chadema
hivyo muda wao wa kuendelea kulikalia
umepitwa kutokana na mbunge
kushindwa kuwatumikia vema
wananchi wa jimbo hilo
wakiwemo vijana ambao waliahidiwa ajira ila hadi leo vijana Iringa mjini wamegeuka
omba omba kutokana na kutokuwa na
ajira .
Hivyo alisema mbali ya
mbunge wa sasa
muda wake kumalizika
bado anapaswa kuwaeleza wananchi
wa jimbo la Iringa mjini matumizi ya fedha za mfuko wa jimbo ambazo amekuwa
akizipata zimefanya kazi gani
katika jimbo hilo lasivyo CCM itakuja na orodha kamili ya
ahadi zake na kiwango halisi cha fedha za mfuko wa jimbo .
Mtenga alisema Chadema
imekuwa ikiendesha siasa
za vurugu kwa
kuwatumia vijana kuvamia
mikutano wa CCM hasa pale wanapoona
wananchi wamejitokeza kwa wingi kwa
lengo la kutaka kuivuruga na
kuwa kuanzia sasa CCM inawaomba vijana hao kuacha
kutumika kwa mashali ya wachache
na kuwa
iwapo watashindwa uvumilivu wa
sera za CCM ni vema wasifike katika katika mikutano badala ya kufika kwa lengo la kufanya fujo.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment