Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe akiteta jambo na askofu wa kanisa Katoliki jimbo la Njombe Mhashamu Alfred Maluma |
Mbunge Filikunjombe akisisitiza jambo wakati akitoa salamu zake kwenye mazishi ya SR. Instrude maria |
Mbunge Filikunjombe katika usikivu mkubwa
Na Matukiodaima BLoG
Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe amewaomba viongozi wa dini nchini kuendelea kuwaombea viongozi wa serikali wakiwemo wabunge ili kuwatumikia wananchi kwa kutanguliza hofu ya Mungu ya kwatumikia wananchi waliowachagua Kauli hiyo aliitoa Jana wakati wa mazishi ya aliyekuwa mtawa wa kanisa la Romanikatoliki Parokia ya Imiliwaa Marehemu SR. Insetrud Maria Alisema kuwa viongozi wa dini wamekuwa wakifanya kazi ya kuliombea Taifa na watu wake ila wanasiasa na viongozi wa serikali wamekuwa wakiwatumikia wananchi kimwili hivyo kuna haja ya viongozi wa dini kuendelea kufanya kazi ya kuwaombea viongozi . " maandiko matakatifu yanasema kuwa enendeni duniani mkawafanyi watu wote kuwa wanafunzi wangu...chama cha walimu hapa wamesema kuwa SR.Maria alikuwa mwalimu mzuri hivyo ni wazi alizifanya kazi zote ya kiroho na Kimwili " Hivyo alisema kwa kutambua mchango wake alioutoa hapa duniani Enzi za uhai wake kwa upande wake ameguswa kujenga darasa katika shule ya sekondari parokioni hapo Kama njia ya kumuenzi zaidi. Filikunjombe alisema kuwa iwapo kitajengwa kitu chochote cha kumbukumbu liwe darasa la shule ya msingi ama sekondari ni kumbukumbu tosha . Alisema mchango wa SR. Maria katika maendeleo ya mkoa wa Njombe ni mkubwa na kuwa haitapendeza mchango wake huo kuachwa bila kuenziwa. " SR .Instrud Maria mbali ya kazi yake ya utawa pia alikuwa ni mwalimu na mchango wake katika shughuli zake ni mkubwa hivyo nawaombeni tumienzi kwa kujenga darasa Moja ambalo litaandikwa jina lake Kama kumbukumbu ya sasa na baadae" Kuwa kwa upande wake atahakikisha darasa hilo linajengwa kwa kupitia uwezo wake na wahisani mbali mbali . SR.Maria alifariki juzi kwa ugonjwa wa shinikizo la Damu na mazishi yake kuongozwa na askofu wa jimbo la Njombe Alfred Maluma . |
0 comments:
Post a Comment