Home » » KAMPUNI YA MAZIWA YA ASAS YAPONGEZA WATEJA WAKE ,SASA YAJA NA MWONEKANO MPYA‏

KAMPUNI YA MAZIWA YA ASAS YAPONGEZA WATEJA WAKE ,SASA YAJA NA MWONEKANO MPYA‏

Furaha ya  bidhaa mpya ya  asas Dairies Ltd  katika  mwonekano  mpya
Hivi ndivyo  maziwa  hayo  yanavyoonekana kwa  sasa 
                                               Na  Matukiodaimablog
Kampuni ya maziwa ya Asas Dairies Limited imewapongeza wateja  wake kwa  kuendelea  kutoa ushirikiano kwa  kutumia bidhaa  zake .

  Afisa masoko wa kampuni ya maziwa ya Asas  Dairies Ltd ya mkoani Iringa Bw Jimy Kiwelu alisema  hayo  leo  wakati akitoa  salam  za mwaka mpya 2015 na  kutambulisha mwonekano mpya  wa  kisasa  zaidi wa chupa  za maziwa  ya kampuni   hiyo kwa  sasa.

Alisema  mbali  ya mafanikio makubwa  ambayo kampuni  hiyo  imefanikiwa  kuyafikia kwa kuendelea kupata tuzo ya  ubora  wa  maziwa  kwa  miaka takribani  miwili  sasa  bado  kampuni  hiyo  imejipanga kuporomoka katika ubora  na katika  kuhakikisha wanaendelea  kushikilia nafasi ya  kwanza na ubora wa maziwa nchini Tanzania   hivi  sasa tayari kampuni hiyo  imekuja na mwonekano mpya  wa maziwa  yake kwa kuwa  katika  chupa tofauti  na zile  za mwanzo .

Hata hivyo  alisema  kuwa  kuanzisha mwonekano  mpya  wa chupa  za maziwa  hayo  kumekwenda   sambamba na  kuongeza  ubora  zaidi  wa  bidhaa  hizo  hivyo kuwakata watumiaji wa bidhaa  zao  kuanza  kufurahia  kuaga mwaka 2014 na  kuukaribisha  mwaka 2015 kwa  kutumia maziwa yenye  mwonekano tofauti na  ule  wa  mwanzo .
                                     Mwonekano  wa  zamani 
Pia alisema kampuni  yake  imekuwa  mbele  katika  kuchangia maendeleo  ya mkoa  wa Iringa kama sehemu ya kutambua ushirikiano mkubwa  wa kampuni kwa maendeleo ya Taifa .

Kiwelu alitaja moja kati ya  shughuli ambazo kampuni imepata  kusaidia kuwa ni pamoja na kuhamasisha  jamii ya  Iringa  na  watanzania  kupenda  kunywa maziwa  kwa afya badala ya  kutumia muda  wao  kuingiza  sumu mwilini kwa kunywa  pombe pia kampuni imepata kutoa  msaada wa madawati yenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 2.7 kwa shule za msingi tatu ambazo zilishinda katika mashindano ya uchoraji wa picha zinazoelezea umuhimu wa unywaji maziwa mashuleni

Mbali ya zawadi hizo kwa shule hizo tatu pia kampuni hiyo ilipata kuwanywesha maziwa wanafunzi zaidi ya 30,000 wa shule za msingi katika Manispaa ya Iringa.

Shule hizo zilizopatiwa msaada wa madawati ni pamoja na Hoho iliyoshika nafasi ya kwanza na kupata madawati yenye thamani ya Tsh milioni 1 ,Mlangali iliyoshika nafasi ya pili na kupata madawati ya Tsh.750,000 pamoja na St Dominic iliyopata madawati yenye thamani ya Tsh 500,000.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa