Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Akikabidhi msaada huo hivi karibuni, Mkurugenzi wa Mkwawa Hunting
Safaris, Ahmed Huwel, alisema kampuni hiyo itaendelea kushirikiana na
Mbomipa na wadau wengine katika kulipa ada na kuwasaidia pale ambako
unahitajika msaada, ili kuhakikisha maliasili katika eneo hilo la
hifadhi zinalindwa na kuvunwa kwa mujibu wa sheria zilizowekwa na
jumuiya hiyo na serikali.
Akipokea fedha hizo kwa niaba ya jumuiya hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya
Mbomipa, Juma Kaundama, aliipongeza kampuni hiyo kwa kujali na kutoa
ushirikiano pale inapoombwa kufanya hivyo.
Alisema jukumu la ulinzi wa maliasili dhidi ya majangili, linagharimu
kiasi kikubwa cha fedha na mara kwa mara kampuni ya Mkwawa imekuwa
ikisaidia jumuiya hiyo katika kutekeleza majukumu yake.
Alibainisha kuwa, kuendesha jumuiya hiyo zinahitajika sh milioni 150
kila mwaka kwa ajili ya kununulia vifaa mbalimbali vikiwemo vya ulinzi,
mikutano na gawio kwa vijiji vinavyounda jumuiya hiyo na mishahara.
Mbomipa ni jumuiya inayoshughulika na uhifadhi wa maeneo ya hifadhi
ya wanyamapori ya jamii (WMA), nje ya mipaka ya Hifadhi ya Taifa ya
Ruaha, wilayani Iringa. Wanyama walioko katika eneo hilo wanatoka ndani
ya hifadhi hiyo na Hifadhi ya Mikumi
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment