Vikundi saba vilivyopo Kata ya Kiwele na
Nduli mkoani Iringa vimekabidhiwa mizinga 100 ya nyuki kwa ajili ya
ufugaji nyuki ili kujikwamua kiumaskini.
Akikabidhi mizinga hiyo kati ya mizinga 120
Mshauri wa Maliasili Mkoa wa Iringa, Aloyce Mawere kwenye mkutano
uliofanyika katika hicho, aliwataka wanakikundi hao kusimamia sheria
zilizowekwa ili kufanikiwa katika ufugaji wa nyuki.
Mawere alisema endapo wanavikundi hao
watafanyakazi kwa ushirikiano na jamii inayozunguka misitu ikiwa ni
pamoja na kuzingatia sheria zilizopo wataona mafanikio na wataachana na
umaskini .
Aliongeza kuwa suala la ufugaji wa nyuki ni ajira
tosha kwa vijana na si wazee tu “Naomba jamii nzima ielimike kwamba
suala la ufugaji siyo kazi ya wazee peke yao pia ni ajira kwa vijana
ambao hawana kazi pamoja na akina mama,hivyo sasa hiyo mizinga
mliopatiwa mhakikishe mnaitumia ipasavyo na mnaifanyia kazi siyo
masnduku ya nguo hayo,” alisema.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment