Mkurugenzi
wa Shirika la Vijana, Walemavu na Watoto (IDYDC) mkoani Iringa, Jonnie
Nkoma akimweleza Katibu Mkuiu wa TFF, Angetile Osia juu ya kituo kipya
cha Iringa Football for Hope Centre kitakachozinduliwa wiki hii ili
kukuza vipaji vya watoto na Vijana mkoani humo. Kushoto ni Mwanachama wa
Tabata Veteran, Ipyana Mwakasege. (Picha na Mpoki Bukuku).
Kituo
cha kisasa cha vijana cha Iringa Football for Hope Centre kinatarajiwa
kufunguliwa mwishoni mwa wiki hii mjini Iringa ikiwa ni sehemu
shamrashamra za uzimwaji wa Mwenge wa Uhuru.
Akizungumza
mjini Iringa juzi Katibu Mkuiu wa TFF, Angetile Osiah alisema kituo
hicho kilichojengwa na Shirika la Vijana, Walemavu na Watoto (IDYDC) la
mkoani Iringa kimefadhiriwa na shirikisho la soka la Kimataifa (FIFA)
ili ukuza vipaji vya mpira na kutoa elimu na ushauri nasaha.
“Mradi
huu haupitii moja kwa moja katika vyama vyetu vya michezo bali katika
taasisi zinazotoa eklimu za kijamii na kufundisha soka” alisema
Angetile.
Alipongeza
shirika la IDYDC kwa kukamilisha mradi huo na kusema kitendo hicho
kitafanya FIFA kutoa fedha zaidi kwa ajili ya miradi kama hiyo nchini.
“FIFA
watafurahi kuiona fedha walizotoa zinatumika ipasavyo kitu ambacho
kitawafanya wawe radhi kutoa misaada zaidi na hii itasaidia kukuza soka
letu”.
Mkurugenzi
wa IDYDC Jonnie Nkoma alimweleza Katibu Mkuu wa TFF kwamab kwa sasa
ujenzi wa kitu hicho uko katika hatua za mwishoni kukamilika na kwamaba
kitaanza kuhudumia timu za watoto na vijana zaidi ya 120
kitakapofunguliwa.
Nkoma
alisema kituo hicho kitakuwa kinatumika usiku na mchana kwani wanafunzi
na watoto watakuwa wakipata mafunzo nyakati za jioni wakati vina na
watoto wa mitaani watatumia usiku kwa ajili ya mazoezi ya kukuza vipaji
vyao.
“Mbali
na michezo vijana watakuwa wanapata mafunzo ya afya ya uzazi na ugonjwa
waUkimwi na pia watapata nafasi ya kujua afya zao kwa kupima Ukimwi
butre hapahapa kituoni.
Mbali
na uwanja kituo hicho kina ofisi, vyumba vya kutoa elimu na ushauri
nasaha, upimaji wa VVU, chumba cha kompyuta na darasa.
Chanzo: Mo Blog
0 comments:
Post a Comment