Mdhamini
mkuu wa mafunzo ya Uigizaji na utayarishaji wa Filamu kwa wasanii wa
mkoa wa Iringa kwa kushirikiana na asasi ya TCDA na shirikisho la filamu
Tanzania (TAFF) Fredrick Mwakalebela.
===== ===== ======
WAIGIZAJI KUPEWA MAFUNZO
Na Denis Mlowe,Iringa
SHIRIKISHO
la Filamu Tanzania(TAFF) kwa kushirikiana na asasi isiyo ya Kiserikali
ya Tanganyika Centre For Development and Advocacy (TCDA) wameandaa
mafunzo ya uigizaji na utayarishaj wa filamu kwa wasaniin wa mkoa wa
Iringa na maeneo ya jirani.
Akizungumza
na Daraja letu mkurugenzi wa asasi hiyo, Jackson Kiyeyeu alisema lengo
la mafunzo hayo ni kuwapa upeo na ujuzi zaidi wasanii wa Iringa katika
kuweza kuandaa filamu bora na kuwa na ujuzi wa katika uigizaji.
Alisema
mafunzo hayo yatakuwa ya mwezi mmoja na yatatolewa na wasanii wakali wa
filamu Tanzania akiwemo msanii nguli Haji Adam maarufu kama Baba Haji
akiambatana na walimu wa sanaa kutoka Dar es Salaam.
Kiyeyeu
alisema wahitimu wa mafunzo hayo watapatiwa vyeti vinavyotambulikana
shirikisho la filamu Tanzania na wasanii bora 10 watapatiwa fursa ya
kushiriki filamu ya No Option itakayochezwa na wakali wa Bongo Movie.
“ Mafunzo
yatatolewa kwa watu wote kuanzia elimu ya shule ya msingi hadi kidato
cha sita na vyeti vitakavyotolewa vitawawezesha kufanya kazi za filamu
popote pale Tanzania na ni wakati wa wasanii sasa kuwa na elimu ya
ugizaji na utayarishaji wa filamu kuliko ilivyo sasa wengi wao kutokuwa
na elimu.” Alisema Kiyeyeu
Mafunzo
ya ugizaji na utayarishaji wa filamu yatakakuwa ni mara ya kwanza kwa
mkoa wa Iringa yamedhaminiwa na aliyekuwa katibu mkuu wa TFF Fredrick
Mwakalebela aliyetoa asilimia 75 ya ada za mafunzo hayo kwa wasanii wa
Iringa.
Kwa
upande wake Daraja Letu lilipozungumza na Mwakalebela alisema lengo ni
kuwasaidia wasanii wa Iringa kuweza kuwa na ufahamu wa uigizaji na
utayarishaji wa filamu bora Tanzania na kuwakomboa vijana katika
umaskini.
Alisema
sanaa ya uigizaji wa filamu una faida kubwa sana katika kuondokana na
tatizo la ajira kwa vijana natoa wito wajitokeze kwa wingi na kuwataka
wadau kuweza kuwasaidia vijana katika kuondokana na tatizo la umasikini
katika kuwaidia kutimiza ndoto zao.
“Kutokana
na kupenda sanaa na michezo kwa ujumla ameguswa sana na wazo la TCDA
kuweza kunipa mawazo yao hivyo sikuwa na budi kuweza kuwadhamini katika
hilo nachoomba wadau wengine waweze kujitokeza kuwasaidia wasanii wa
Iringa kuweza kutambulika kitaifa na kimataifa katika tasnia ya Filamu.”
Alisema Mwakalebela
Alisema
Iringa kuna wasanii wengi wanaojitahidi kupambana kwa uwezo wao binafsi
kufanya sanaa kwa kile anachofikiria bila elimu ya sanaa ya ugizaji na
utayarishaji wa filamu.
Mwakalebela
alisema wasanii watakaofanya vizuri katika mafunzo hayo watashirkishwa
katika filamu mbalimbali ambazo zinaandaliwa na wasanii wakubwa kutoka
jiji Dar es salaam kwa lengo la kuwainua mbeleni waweze kujitegemea.
0 comments:
Post a Comment