MKUU wa Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa Mh. Gerlad Guninita ameomba
kupatiwa ulinzi madhubuti, baada ya kupokea vitisho vinavyoashiria
hatari ya uhai wake, hatua inayotokana na kuwaadabisha kwa kudhibiti
mienendo mibovu ya baadhi ya watumishi wa Halmashauri hiyo ya kilolo
ambao wamekuwa wakikaidi kutekeleza majukumu yao.
Akizungumzia wasiwasi wa hatari hiyo katika kikao cha baraza la
madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo mkoni Iringa, Guninita
amesema amekuwa akipata vitisho baada ya kutoa adhabu kwa watumishi
mbalimbali wilayani humo huku baadhi yao wakidiliki kumtumia njia ya
ujumbe wa Simu, hatua inayoashiria maisha yake kuwa hatarini, jambo
linalosababisha kuishi kwa mashaka na kulazimika kufungua jalada
polisi lenye namba IR/RB/1799/2013 katika kituo cha Polisi Iringa.
Guninita amesema baadhi ya watumishi wamemchukia zaidi baada ya kubana
njia za ubadhilifu wa fedha za umma, na kupinga utaratibu wa baadhi ya
watumishi kuishi Iringa mjini umbali wa zaidi ya km 40 na kusababisha
kuchelewa kufika kazini huku kukiwa na matumizi holela ya magari na
mafuta, kwa kuwa watumishi hao hupelekwa Kilolo na kurudishwa tena
Iringa mjini, jambo linalochangia ufujaji mkubwa wa fedha za
wananchi, fedha ambazo zingefanya shughuli za kiuchumi.
zaidi msikie hapa
0 comments:
Post a Comment