HATIMAYE wanafunzi wa
jamii ya wafugaji, wanaosoma katika vyuo vikuu mkoani Iringa, wameungana na
kutoa tamko juu ya mgogolo wa Loliondo mkoani Arusha, huku wakimtaka waziri
mwenye dhamana ya maliasiri na Utalii, Barozi Hamis Kagasheki huku kurejea upya
namna ya kutatua mgogolo huo.
Tamko hilo limetolewa na
umoja wa wanafunzi wa vyuo vikuu wanaotoka katika jamii ya wafugaji, na
akisoma tamko la wanachuo hao Solomon Lekui amesema kamwe wao hawapo
tayari kushuhudia wazazi wao wakipokonywa ardhi ambayo ni mali yao halali.
Lekui
amesema serikali inapaswa itafakari zaidi suala la wafugaji kitaifa, kwa kuunda
Tume maalumu ya kukusanya maoni ya wafugaji kote nchini katika kutafuta
namna ya kutatua kikamilifu migogolo, kwa kuwashirikisha wafugaji wenyewe
ili wapate fulsa ya kubainisha changamoto na matatizo yanayowakabiri.
Emmanuel
Ole Kileli mwanafunzi kutoka chuo kikuu cha Tumaini amesema imekuwa kama
desturi kwa wafugaji kulalamika mambo mbalimbali yanayohusiana na unyang’anyi
wa ardhi yao inayoambatana na uhamishaji kwa kutumia nguvu na upotevu mkubwa wa
mali na maisha yao.
amesema
Serikali imekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza maamuzi magumu kwa wafugaji
nchini, kwa madai kuwa wafugaji wanakiuka sheria kwa kuvamia maeneo mbalimbali
yasiyo ya ufugaji hasa maeneo ya hifadhi naya kilimo, na kuwa hatua hiyo ni
kutokana na kukosekana kwa sera ya ufugaji asili (Pastoralism Policy)
ambayo ingehusika kuratibu na kuthamini shughuli mbalimbali za ufugajiasili na
mazao yake kwa ujumla.Wamesema serikali itambue wafugaji nao wanayo haki kama
walivyo watanzania wengine, na sasa kuna haja ya kutoa vipaumbele sawa kwa
kundi la wakulima na wafugaji.
Saikoni
Justin mwenyekiti wa umoja wa wanachuo wanatoka katika jamii ya
wafugaji, amesema kuna ukiukwaji wa sheria za kimataifa katika uchukuaji wa
ardhi ya Loliondo na wao kama wamesomeshwa na mifugo na wanayo haki ya kutetea
jamii yao, huku akiitaka serikali kuacha Propaganda ambazo hazina
maslahi wala tija kwa wananchi wake, na badala yake itumike busara katika
utatuzi wa migogolo pasipo kuingiza masuala ya Siasa.
0 comments:
Post a Comment