Home » » PICHA YA BINTI WA MIAKA 16 ALIYELAZIMISHWA KUNYWA MKOJO NA MAMA YAKE MDOGO HUKO IRINGA

PICHA YA BINTI WA MIAKA 16 ALIYELAZIMISHWA KUNYWA MKOJO NA MAMA YAKE MDOGO HUKO IRINGA








Vituko
mjini Iringa haviwezi kuisha kama jamii haitakubali kwa moyo mmoja
kupambana na ukatili wa kijinsia. Huyu ni Binti ZAWAD KARIM miaka 16
mkazi wa mshindo nyuma ya banki ya NBC manispaa ya Iringa amepigwa na
hatimaye kunyweshwa mkojo na mama yake mdogo aitwaye Ever ubamba.
Tukio lilikuwa hivi:
Zawadi
kimsingi anaishi na mama yake mzazi ambaye kwa kipindi hicho dada mtu
huyo alikuwa anaumwa. Ever alikuwa nje na marafiki zake ndipo mama yake
mdogo huyo akamwiita ndani ya nyumba yao hiyo wanayoishi mtaa wa
mshindo.
Baada
ya kumwita na kisha mtoto huyo kushindwa kusikia baadaye aliitika na
kuingia ndani na  ndipo alipo ambiwa avue nguo zote na huyo mama yake 
mdogo Ever .Baada ya muda mfupi Zawadi alianza kupokea kipigo kikali
kutoka kwa mama yake  mdogo.
Katika
kipigo hicho Zawadi  alipigwa pamoja na kunyweshwa mkojo kutoka kwa
mama yake mdogo huyo.Zawadi ambaye ni mtoto wa kuzaliwa na Dada yake
Ever inadaiwa kipigo hicho kimesababishwa na tuhuma kwamba eti familia
hiyo haina mtoto kama yeye zawadi.

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa