Home » » LOWASSA kukabidhiwa tuzo ya heshima Iringa jumapili

LOWASSA kukabidhiwa tuzo ya heshima Iringa jumapili


WAUMINI  na uongozi  wa  huduma   ya injili na uponyaji  ya Overcomers Power
Center  (OPC) chini ya Askofu Dkt Boaz Sollo inategemea  kumtunuku  tuzo ya 

heshima kwa mchango  wake mkubwa katika Taifa waziri mkuu  mstaafu  wa jamuhuri ya  Muungano  wa Tanzania Edward Lowassa katika  hafla  maalum  itakayofanyika  siku ya 
jumapili mjini  Iringa .


Waumini  hao  wameandaa maandamano makubwa  ya amani  kwa  ajili ya  kumpokea Lowassa  kutoka  katika  uwanja  wa Ndege Nduli  majira ya saa 3 asubuhi  atakapowasili kwa Ndege na  kuelekea katika  ukumbi  wa St Dominic ambako kutafanyika  shughuli  hiyo kuanzia muda wa saa 6 mchana .



Akizungumza na  waandishi  wa habari leo  askofu Dkt Sollo  alisema  kuwa mbali ya 
kumtunuku tuzo  hiyo  Bw Lowassa pia  kiongozi  huyo anataongoza  harambee ya  kuchangia ujenzi wa  jengo la kanisa  la OPC linaloendelea  kujengwa katika  eneo la zizi la Ng’ombe ambapo  zaidi ya  Tsh. Milioni 250 zinahitajiika kukamilisha  ujenzi wa  jengo hilo  pamoja na kituo cha Radio   Overcomers Fm (98.6 Mhz)kilichopo mjini Iringa .



Dkt  Sollo  alisema kuwa  lengo la  OPC kumwalika na kumtunuku  tuzo ya  heshima  Bw 
Lowassa ni  kutokana na kuwa  jirani zaidi na jamii na amekuwa akiitika wito  wa makundi mbali mbali  na kuyasaidia bila  ubaguzi wowote  hivyo kutokana na mchango  wake huo kwa jamii wao  kama kanisa wameona ni  vema  kuutambua mchango  wake huo na kumwalika  ili kumpa tuzo hiyo maalum kama ahsante kwake.


“ Tuzo  hiyo  itampa moyo zaidi  wa kuendelea  kuwa karibu na jamii na  kutambua pia mapokeo ya  jamii ambayo amekuwa akiisaidia mara kwa mara….ikiwa ni  pamoja na  kuendelea 
kusaidia  kuendeleza amani nchini kwa kuchangia nyumba  za ibada”


Pia  alimtaka Lowassa  kuendelea  kusaidia jamii bila  kuchoka hata kama baadhi ya  watu 
wasiopenda jitihada zake kuendelea   kutoa maneno yenye  kumkatisha tamaa na kuwa siku  zote kile anachokifanya  jamii inakitambua na Mungu ndie ajuaye na ndie mtoa baraka kwake.


Dkt  Sollo  alisema kuwa Lowassa ambae ni mbunge wa  jimbo la Monduli mkoani Arusha  amekuwa kipenzi cha  wengi hata wale  wasio wapiga  kura wake na  kuwa  uongozi wake kama  waziri  mkuu wengi  walitokea  kumpenda na kuwa toka alipojiuzulu nafasi  hiyo ya  uwaziri mkuu hajapata  kufika mkoani Iringa  hivyo sehemu kubwa ya  wana Iringa wana hamu  kubwa ya  kukutana nae kwa mara  nyingine.


Hata  hivyo  baadhi ya  wakazi  wa Manispaa ya  Iringa wamepongeza  hatua ya OPC chini ya
Dkt Sollo kuamua  kumtunuku  tuzo hiyo Lowassa na  kuwa ni kweli anastahili  kupewa  tuzo kwani ni miongoni mwa viongozi  waadilifu na  wachapa kazi hapa nchini.


Anania  Sanga  alisema kuwa  kuna kila  sababu ya viongozi kama  Lowassa kuendelea  kuthiaminiwa kama  ambavyo OPC ilivyoamua  kuutambua mchango  wake kwa  kukusudia 
kumtunuku tuzo hiyo maalum ambayo si heshima kwa  kituo hicho  cha OPC pekee 
bali ni heshima ya  mkoa  wa Iringa ni mfano  kwa viongozi  wengine  kufanya kazi 
ya jamii  kwa ufanisi zaidi  ili kuja  kupongezwa na jamii kama  hivyo .

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa