Home » » WANANCHI IRINGA WALISHWA MZOGA ,MUUZAJI ATIMUA MBIO,TAZAMA HAPA

WANANCHI IRINGA WALISHWA MZOGA ,MUUZAJI ATIMUA MBIO,TAZAMA HAPA



Vijana  wakionyesha kaburi ambalo mzoga huo  wa ng'ombe ulizikwa likiwa na mabaki ya nyama
Haya ni mabaki ya mzoga huu baada ya  kuzikwa tena leo

TABIA ya baadhi ya wakazi wa mkoa wa Iringa kupenda nyama nyama bila kuangalia ni wapi wanakula ama kununua nyama hiyo ,imewatokea puani wakazi wa Ikonongo kata ya Mkwawa katika Manispaa ya Iringa baada ya kuuziwa nyama ya mzoga wa ng'ombe aliyekufa kwa  sumu toka usiku wa jana.

Wananchi hao   wamejikuta katika  majuto baada ya kujisikia dalilia  za matumbo  kuuna baada ya  kufakamia nyama  hiyo ya mzoga kwa  zaidi ya  siku  mbili  sasa.

wakizungumza na mtandao  huu  wa www.francisgodwin.blogspot.com leo baadhi ya  wafanyakazi  wa shamba la mifugo la raia  wa nchini China ambao  walishuhudia  kifo cha ng'ombe huyo na kuzikwa kwake ,walisema  kuwa ng'ombe huyo  alikufa toka jana na  kuzikwa baada ya  kuchukuliwa  vipimo na kuonekana kifo  chake  kimesababishwa na  sumu .

Bila  kutaja aina ya  sumu  iliyopelekea kifo cha ng'ombe huyo  walidai kuwa  baada ya  kupimwa lilichimbwa  shimo  kubwa na  kufukia mzoga  huyo huku mwenzao huyo akionyesha  tamaa kwa  kuwaomba  wasifukie  sana mzoga  huyo.

Hata  hivyo  baada ya  kukamilisha  zoezi la  kufukia mzoga  huyo inadaiwa  kuwa mwenzao  mmoja aliyefahamika kwa  jina la Abdu alirudi  usiku na kufukua mzoga  huyo na  kumchunja  ngozi kisha kupeleka kijiji  kufungua  bucha la nyama na  wananchi  wa  eneo hilo kuchangmkia  kununua nyama  hiyo ya bei ya  kutupwa .

Salome kalinga ni mmoja kati ya  wakazi  wa Ikonongo ambae  alipata  kula nyama  hiyo amesema  kuwa bei ya kutupwa ambayo nyama  hiyo  ilikuwa ikiuzwa ndio  iliwasukuma  wananchi wengi kuchangamkia nyama  hiyo na hata  kununua ya  kutosha kwa kwenda  kuweka akiba majumbani kwao.

"Sisi tuliambiwa  kuwa mchina huyo ameamua  kutoa sadaka kwa  wakazi hao kwa  kumkubali  kuwa muwekezaji katika  eneo hilo  hivyo kilo la nyama badala ya kuuzwa shilingi 5000 kama ilivyo buchani  kijana  huyo  alikuwa akiuza shilingi  2000 hadi 1000 na iwapo unapungufu unaongea"

Alisema  kuwa baada ya  kula nyama  hiyo kwa  siku mbili mfululizo  sasa ndipo  leo wamebaini  kuwa nyama hiyo  si nyama tena bali ni mzoga na hivyo kuamua  kufanya msako na  kufanikiwa  kuwakamata  wauzaji wawili akiwemo kijana  huyo ambae baadae alitoweka.

Hivyo  hadi sasa  kijana mmoja  amekamatwa akiwa na nyama  kilo 10 ambazo alikuwa akiendelea  kuuza na kupewa  kichapo kabla ya  kupelekwa  polisi.

Tabia ya  wananchi wa Iringa kuchangamkia mishkaki na nyama ambayo  inauzwa kwa  bei ya  kutupwa imeendelea  kukua na hivyo ili kuepuka  kulishwa mizoga ni vema tahadhari zaidi  kuchukuliwa na  walaji nyama.
Na Francis Godwin

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa