Bi.Jesca Msambatavangu mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa
MWENYEKITI wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu amempongeza Rais Dkt Jakaya Kikwete kwa kuendelea kudumisha amani ya taifa na kuwataka a wana CCM mkoani Iringa na nchini kote kuendelea kudumisha amani na mshikamano na kuepukana na siasa vya vurugu ili kuendelea kumuunga mkono Rais Dkt Kikwete na kumuenzi hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere katika kudumisha amani ya Taifa letu.
Akiwahotubia wana CCM wa tawi la Mkwajuni kata ya Nyanzwa tarafa ya Mahenge wilaya ya Kilolo mkoani Iringa jana katika maadhimisho ya miaka 36 ya kuzaliwa kwa CCM,Msambatavangu alisema kuwa kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi kulilenga kukuza demokrasia nchini ila sasa vyama vya siasa hasa vyama vya upinzani vimegeuza siasa ni ulingo wa matusi na vurugu jambo mbalo ni kinyume na malengo sahihi ya kuanzishwa kwa mfumo huo wa vyama vingi nchini.
Hivyo alisema ni heri kubaki na chama kimoja ambacho kimelifikisha hapa lilipo bila watu kugombana wala kumwaga damu badala ya kuendelea kutaka kuwa na serikali ya vyama ambavyo vimeshindwa kulinda amani yetu na kuendelea kulichafua Taifa kwa vurugu aza kisiasa zisizo na ukomo jambo ambalo ni hatari kama litaendelea kupewa nafasi katika jamii yetu
Msambatavangu alisema vyama vya upinzani vimekuwa ni chanzo cha kuanzisha fujo katika mikutano ya CCM na kuwa kutokana na mbinu hizo chafu hivi sasa CCM imejikita zaidi katika kuwaeleza wananchi utekelezaji wa ilani yake badala ya kuanza utekelezaji wa ajenda za baadhi ya vyama vya siasa ambavyo wakati wote kwao vurugu ni kama mtaji wa kisiasa.
Hata hivyo mwenyekiti huyo wa CCM mkoa wa Iringa aliwataka wana CCM kuendelea kuendesha siasa kwa kuzingatia amani ya Taifa na kila wanapotimiza wajibu wao kujaribu kujikumbusha misingi ya amani na utulivu iliyoachwa na mwalimu Nyerere na jitihada zinazoendelezwa na mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt Rais Kikwete katika kudumisha amani ya Taifa letu.
Alisema kuwa mwenyekiti wa CCM Dkt Kikwete amekuwa ni kiongozi wa mfano kwa Taifa katika kuliongoza Taifa kwa misingi ya baba wa Taifa hayati Nyerere na kuwa wakati wote Dkt Kikwete amekuwa akikemea vitendo vya uchochezi na uvunjifu wa amani ya Taifa vinavyofanywa na baadhi ya viongozi wa vyama vya kiasia hapa nchini .
Alisema kuwa kila mtanzania anayo nafasi ya kumsaidia Rais Kikwete katika kupigania amani ya Taifa na kujiepusha na vyama vya siasa ambavyo vipo kwa ajili ya kuvuruga amani ya Taifa na kuwa iwapo Taifa litakosa amani na utulivu si wana CCM peke yao ambao watayakimbia makazi yao ila ni wananchi wote wataishi maisha ya kuhangaika kama ilivyo leo Somaria na Ethiopia ambako Raia wake kila kukicha wanayakimbia makazi yao.
"Ndugu zangu kama tumefanikiwa kufika hapa tulipo leo kwa CCM kuadhimisha miaka 36 bila kumwaga damu na tumeruhusi mfomo wa vyama vingi ambavyo vinaendelea kuchochea vurugu ....kuna haja gani ya kujiunga na vyama visivyopanda amani na kuachana na CCM kilichoweza kulinda amani.....nawaombeni tusiyumbishwe na bendera za vyama tuendelee kubaki CCM" alisema Msambatavangu
Akielezea kuhusu CCM ilivyoendelea kutekeleza ilani yake katika sekta ya Kilimo alisema kuwa Kilimo ni moja kati ya sekta tegemeo kubwa kwa uchumi wa Taifa hivyo lengo ni kujenga Uchumi wa kisasa utakaopelekea Taifa letu kujitegemea.
"Sasa kama wengine wanazalisha mbegu bora, wauzaji wanachakachuka, wakulima wanapewa mbegu na mbolea za ruzuku wanauza vocha, Vyuoni hakuna utafiti wakutosha kusaidia mapinduzi haya ya kilimo ni tatizo katika kufikia mpango wa maendeleo wa Taifa letu"
Alisema hivyo Serikali ya CCM kupitia Ilani yake ya mwaka 2010-2015 inalengo la Kuongeza KASI ya ujenzi wa Uchumi wa Kisasa na Taifa linalojitegemea kwa kuwashirikisha na kuwawezesha kiuchumi wananchi.
Msambatavangu alisema katika kufikia malengo hayo ya Kuongeza maarifa na matumizi ya sayansi na Teknolojia katika sekta za Uzalishaji wakulima wameendelea kusaidiwa mbinu na pembejeo za ruzuku Ili kuongeza Uzalishaji,Ufanisi na Tija au faida katika uchumi hususani katika Kilimo .
Na Francis Godwin
Na Francis Godwin
0 comments:
Post a Comment