Home » » MWANAFUNZI AFA KWA KUANGUKIWA NA UKUTA WAKATI AKIPITA NJIA ZA PANYA KUONA MTIKISIKO IRINGA

MWANAFUNZI AFA KWA KUANGUKIWA NA UKUTA WAKATI AKIPITA NJIA ZA PANYA KUONA MTIKISIKO IRINGA





Sehemu  ya ukuta  uliobomoka
                   Sehemu ya ukuta  iliyobomoko na kusababishaa  kifo cha mwanafunzi mmoja
Wasamaria  wema wakijaribu kumwokoa kijana aliyeangukiwa na ukuta kwa  kufukua kifusi kwa mikono

Mwanafunzi  wa  kidato  cha pili katika  shule  ya sekondari  Kwakilosa katika Manispaa ya  Iringa  Daniel Yona (15) amefariki  dunia baada ya  kuaungukiwa na ukuta  wa uwanja  wa Samora wakati akijaribu kupita mlango  wa panya  ili kwenda  kushuhudia tamasha  hilo la Mtikisiko 2012.


Tukio  hilo  lilitokea usiku  wa kuamkia Desemba 2 mwaka huu wakati wapenda  burudani katika mkoa wa Iringa  walipofika katika uwanja  huo kushuhudia onyesho kubwa la Mtikisiko 2012 ambalo  lilikuwa limepambwa na  wasanii mbali mbali  wakiongozwa na mkongwe Juma Nature na Profesa J.

Wakielezea  kilichomkuta mwanafunzi huyo baada ya mashuhuda  walisema  kuwa mwanafunzi  huyo na wenzake  waliacha kupita katika mlango  wa kawaida kwa  kulipia kiingilio halali  kilichowekwa na badala yake  aliamua  kupita gizani na kupanda ukuta  huo  wa uwanja  wa Samora  ili kuweza  kuingia ndani ya  uwanja  huo kuona tamasha la Mtikisiko.

Hata  hivyo mmoja kati ya mashuhuda ambae hakupenda  kutajwa  jina lake hapa alisema kuwa kabla ya  mwanafunzi huyo kupanda ukuta  huo  kuna  vijana kama 20 ambao  walifanikiwa  kupita eneo  hilo bila  kulipa  kiingilio na baada ya  kufanikiwa  kupita  walianza  kupigiana simu huku baadhi ya  vijana  wa kitanzini   wakiwatoza vijana hao  wanaoruka  ukuta  kiingilia cha  shilingi 1000 hadi shilingi 500 .

"Ujue hapa vijana  wa kihuni kutoka  Kitanzini  walikuwa  wamejipanga hapa na  kufanya ufisadi wa kuwatoza  watu kiingilio bila  wahusika wa Tamasha  hilo kujua  kinachoendelea  .....hivyo hata  huyo mwanafunzi alikuwa ni mmoja kati ya  wavamizi  wa Tamasha  hilo kwa  kupita njia ya panya  ili  kuingia ndani ya  uwanja huo"

Pia alisema ukuta  huo  ulionyesha  kuzidiwa  nguvu kutokana na ubovu  wa ukuta  wenyewe kuwa ni mbovu na ulikuwa  umeungwa  kienyeji katika  eneo hilo .

Aidha  alisema  baada ya  vijana zaidi ya  watano  kupanda  eneo  hilo la ukuta ambalo lipo upande  wa kushoto mwa uwanja  huo wa uwanja ukuta  huo  ulionyesha  kuyumba na kupelekea  vijana  wengine  kuruka na kumwacha  mwanafunzi huyo ambae tayari alikuwa  ameingiza mguu mmoja ndani ya uwanja na mguu wa  pili  ulikuwa nje. 

Alisema baada ya  ukuta  huo kuanguka na kumfunika  walifanikiwa  kumwokoa akiwa hai na kumkimbiza  Hospitali ya mkoa  wa Iringa ambako asubuhi ya siku ya pili ya Desemba 2 majira ya saa 5 asubuhi  alifariki  dunia.

Hata  hivyo askari  polisi  waliokuwepo  eneo  hilo la tukio  walimthibitishia mwandishi  wa mtandao  huu kuwa ni kweli kijana  huyo amefariki  dunia japo  wao si  wasemaji  wa jeshi la polisi na kudai  kuwa chanzo ni kijana  huyo mwenyewe  kutaka kupita mlango  wa panya na kuacha  kupita mlangoni ambako watu  wote  walikuwa  wakipita bila kupata matatizo yoyote.

Hata hivyo uchunguzi wa mtandao  huu  unaonyesha  kuwa  kifo cha mwanafunzi  huyo kimesababishwa na mwanafunzi mwenyewe  kutokana na kutaka  kupita njia ya panya na kuacha mlango  kwani iwapo angetumia njia sahihi  kuingia uwanjani yawezekana kifo kisingeweza kutokea .

Source: Francis Godwin Blog

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa