Home » » WANAFUNZI SEKONDARI YA SADANI WALIA CHAKULA NJE, GIZANI

WANAFUNZI SEKONDARI YA SADANI WALIA CHAKULA NJE, GIZANI

Mwandishi wetu, Iringa Yetu

SHULE yan Sekondari Sadani Iliyopo Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa inakabiriwa na changamoto za ukosefu wa miundo mbinu, bwalo la kulia chakula na nishati ya umeme.

Hayo yamebainishwa wakati wa maharari ya 26 yaliyofanyika shuleni hapo ambapo changamotoi hizo zinasababisha wanafunzi kushinwa kujisomea wakati wa usiku.

Akisoma taarifa ya shule hiyo kwa mgeni rasimi mkuu wa shule hiyo Mw. Benedict Baso alisema, suala ukosefu wa bwalo la shule ni limekuwa sugu ambalo linahitaji ufumbuzi wa haraka zaidi.

Mw. Baso alisema, kutokuwepo kwa bwalo la shule hali hiyoinasababisha usumbufu kwa wanafunzi ambao wanakaa bweni kukosa nafasi ya kulia chakula na kwamba katika vipindi vya mitihani ya taifa hulazimika kutumia vyumba vitano hadi sita kwa wanafunzi 200 waliopo.

Mgeni rasmi katika mahafari hayo Bw. Exaud Kigahe kutoka wizara ya viwanda na biashara amewataka wanafunzi hao wajiandae vema waweze kufaulu mitihani yao ili waweze kuendelea na elimu ya juu.


Mwakilishi wa wazazi Bw. Augustino Mbedule amewaasa wanafunzi hao kutobweteka, baada ya kuhitimu elimu ya sekondari badala yake watumie elimu waliyopata kujiendeleza kimaisha pamoja na kuwasaidia wazazi shughuli mbalimbali za kiuchumi.
Blogzamikoa

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa