Mtandao wa mashirika yasiyo ya kiserikali katika mkoa wa Iringa(ICISO -UMBRELLA) kwa kushirikiana na mitandao ya AZAKI ya halmashauri ya manispaa ya Iringa (IMUCISO) na Iringa Vijijini (IRUNGO) na wilaya ya Kilolo (KIDINGOU) wanatarajia kufanya mdahalo wa haki na fursa sawa kwa jinsia zote katika wilaya hizo.
Mwandishi wetu Denis Mlowe anaripoti kutoka Iringa kuwa akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake katibu mtendaji wa ICISO-UMBRELLA
Raphael Mtitu (pichani akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani) amesema kwamba lengo la mdahalo huo ni kuongeza uewelewa kwa wananchi kuhusu umuhimu wa haki na fursa sawa kwa jinsia katika mkoa wa iringa na wilaya zake kwa ujumla."lengo ni kuwapa wanajamii uelewa juu ya haki za kijinsia na kupunguza matukio ya ubaguzi na unyanyasaji wa kijinsia katika ngazi mbalimbali katika kaya,familia na jamii.
Aidha mdahalo hiyo itakayofanyika tarehe tofauti na ukianza na jimbo la kilolo tarehe 6 mwezi huu katika shule ya sekondari image na kufuatia jimbo la ismani katika ukumbi wa christopher itunundu tarehe 10 ni muendelezo wa mradi wa kuimarisha mahusiano kati ya wananchi na wawakilishi wao ambao unatelekezwa kwa njia ya midahalo.
walengwa wa midahalo hiyo ni wananchi wote na wanaombwa wajitokeze kwa wingi kwa lengo la kupata elimu hiyo ya fursa sawa kwa jinsia zote.
0 comments:
Post a Comment