Home » » MTOTO JULIANA MWINUKA LEO KUFANYIWA OPRESHENI CCBRT

MTOTO JULIANA MWINUKA LEO KUFANYIWA OPRESHENI CCBRT


Mtoto  Juliana Mwinuka
Majeraha  yaliyotokana na kuungua moto klatika  uso wa mtoto  mtoto  Juliana Mwinuka (16) mkazi  wa kitongoji cha Ushindi kata ya Mavanga  wilaya ya  Ludewa  mkoa  wa Njombe yameanza kuziba taratibu huku leo anategemea  kukutana na madaktari bingwa duniani ambao  wamewasili katika Hospitali ya CCBRT .

Kila mmoja  wetu tunaomba aendelee  kumwomba Mwenyezi Mungu kwa  dini yake ili kuweza  kutenda miujiza  ili mtoto  huyo aweze kupona.

 Mtandao huu unaendelea kuwapongeza wote wanaoendelea kuguswa na kuungana na wadau wengine kumchangia fedha za matibabu ,mtoto Juliana kama anavyoonekana akiwa ameunga uso wake kwa moto ni yatima anahitaji msaada wako ili kunusuru maisha yake waweza kutuma mchango wako kwa njia ya M-PESA katika namba hii 0754 026 299 au Tigo Pesa 0712 750199 namba hizi ni za mmiliki wa Bw Francis Godwin

Nawaomba tuungane kufanikisha kuokoa maisha ya mtoto Juliana Mwinuka na Mungu atatuongezea zaidi

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa