Home » » WAISLAM WATAKIWA KUENDELEZA MATENDO MEMA

WAISLAM WATAKIWA KUENDELEZA MATENDO MEMA


Na Mwandishi wetu, Iringa.
WAUMINI wa dini ya kiislam Mkoa wa Iringa na nchini kwa jumla wameaswa kuendeleza mema hata baada ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kumalizika.

Wito huo umetolewa na Ustaadhi Muhibu Senga wakati akitoa hotba ya Idd El Fitr katika swala ya pamoja ya Idd iliyofanyika katika uwanja wa mpira wa miguu wa samara na kuwajumuisha karibu waislam wote wa Manispaa ya Iringa.

Swala hiyo iliyoanza majira ya saa mbili asubuhi leo imeongozwa na Ustaadhi Salim Suleiman na kuhudhuriwa na maelfu ya waislam wa Manispaa ya Iringa na viunga vyake.

Ustaadhi Senga amesema waislam ambao wataachana na misikiti na kuanza kutenda maovu baada ya mfungo mtukufu wa Ramadhan, funga yao yote itakuwa ni sawa na bure.

Akizungumza na waadishi wa habari baada ya swala hiyo, Shekh wa Mkoa wa Iringa,Shekh Ally Juma Tagalile ameto wito kwa waislam wote nchini kushiriki zoezi la sensa ya watu na makazi linalotarajiwa kuanzia usiku wa Agosti 25 na kuendelea kwa siku saba baadaye.

Blogzamikoa

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa