Home » » WAANDISHI WANOLEWA KUHUSU UCHUNGUZI

WAANDISHI WANOLEWA KUHUSU UCHUNGUZI


na Francis Godwin, Iringa
WAANDISHI wa habari mkoani Iringa wameanza kupatiwa mafunzo ya uandishi wa habari za uchunguzi ili kuwawezesha kuongeza ujuzi zaidi katika kuitumikia tasnia hiyo.
Katibu mtendaji wa klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Iringa ( IPC) Frank Leonard, alisema jana  kuwa mafunzo hayo ya siku sita kwa waandishi wa habari wanachama wa IPC yanatolewa na umoja  wa vilabu vya waandishi wa habari Tanzania ( UTPC) kupitia ufadhili wa serikali ya Sweden kupitia Shirika lake la Maendeleo la Kimataifa ( SIDA).
Leonard alisema kuwa mafunzo hayo yanatolewa na Mkufunzi Nyaronyo Kicheere, mwanahabari na wakili wa kujitegemea nchini, yatawasaidia wanahabari hao kuongeza ufanisi katika utendaji wao ili kuviongezea heshima vyombo vyao wanavyofanyia kazi.
Pia alisema pamoja na wanahabari wengi hapa nchini kuandika habari mbali mbali za kiuchunguzi zimekuwa zikiandikwa kwa uchache.
Alisema kuwa kutolewa kwa mafunzo hayo kutamwezesha mwanahabari kuandika habari zenye uhakika baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kutosha .
Kwa upande wake mkufunzi huyo, aliwaeleza wanahabari hao kuwa sifa kubwa ya kuwa mwandishi wa habari za uchunguzi ni kujenga heshima katika jamii na kusaidia wananchi kupata uelewa wa mambo katika maeneo yao.
Chanzo: Tanzania Daima

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa