Home » » RC IRINGA AWATAKA WAJUMBE WA UWT -CCM KUACHA KUTEUA MAJINA YA WAGOMBEA KWA MISINGI YA UDINI NA UKABILA

RC IRINGA AWATAKA WAJUMBE WA UWT -CCM KUACHA KUTEUA MAJINA YA WAGOMBEA KWA MISINGI YA UDINI NA UKABILA


Mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt Christine Ishengoma
Mkuu wa mkoa wa Iringa DKT Christine Ishengoma awataka wajumbe wa umoja wa wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Iringa kutenda haki katika kutoa mapendekezo yao kwa wanachama waliogombea nafasi mbali mbali badala ya kufanya uteuzi kwa misingi ya ukabila ,udini na urangi badala yake kutazama sifa za wagombea.

Mkuu huyo alitoa kauli hiyo leo katika ofisi za CCM mkoa wakati akifungua kikao cha mapendekezo ya wagombea walioomba nafasi mbali mbali ngazi ya wilaya hadi Taifa.

Alisema kuwa idadi kubwa wamejitokeza kugombea ila cha Msingi ni kutazama wale wenye uwezo wa kuhamasisha ,asiwe mpenda makundi ama mwenye kutanguliza maslahi yake badala ya kutazama Chama.

DKT Ishengoma alitaka wajumbe hao pia kuwatakaa viongozi wapenda Rushwa ili kukifanya Chama kuendelea kuwa hai na kuwa Chama chenye viongozi wa mfano kwa vyama vingine vya siasa.

Mkuu wa mkoa ambaye pia ni mbunge wa viti maalum (CCM) mkoa wa Morogoro bado alisema kuwa CCM itaendelea kufanya vema iwapo jumuiya zote za CCM zitafanya kazi kwa pamoja .

Hata hivyo alisema lazima kiongozi anayechaguliwa ni yule mwenye kuwaibika vema na asiyewajibika asipewe nafasi katika jumuiya na Chama Kwani lazima Kiongozi aliyejitokeza kuomba tena lazima kujiridhisha na utendaji wake kwanza Kama hakufanya vema asipewe nafasi.

Akishukuru kwa niaba ya Wanawake hao mjumbe Anna Msolla alisema kuwa mbali ya mkuu huyo wa mkoa kuwaasa Wanawake hao bado alisema kuwa wajumbe hao hawatafanya makosa katika kuteua wajumbe wenye sifa.

Kwani alisema kuwa ili CCM iweze kufanya vema na kutoa ushindani kwa vyama vya upinzani lazima kufanya vema katika uchujaji wa majina.

Kuhusu zoezi la sensa ya watu na makazi linataraji kufanyika usiku wa Agosti 25 kuamkia Agosti 26 mwaka huu mkuu huyo wa mkoa aliwataka wanawake hao kufanya kazi ya kuwahamasisha wenzao ili kujitokeza katika zoezi hilo . Pia alisema kuwa suala hilo la sensa la lile la katiba halina chama hivyo vyama vyote wanapaswa kushiriki mazoezi hayo mawili .

Awali mkuu wa wilaya ya Iringa DKT Leticia Warioba aliwataka Wanawake kuacha kutegemea kuwezeshwa kwa kila jambo na badala yake kusimama kutetea nafasi mbali mbali bila kungoja kuwezeshwa .
Chanzo Francis Godwin

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa