mmiliki wa mtandao wa mzee wa matukio daima akiwa katika ufukwe wa ziwa Nyasa eneo la Manda
Tunasubiri kwenda kufanya kazi ya kulinda mpaka wetu kati ya Tanzania na Malawi
Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa amani na Utulivu hivyo bado watanzania tunawajibu wa kuendelea kulinda amani yetu na hata kuombea amani tuliyonayo ili iendelee kuheshimika.
Nimepatwa na hofu juu ya kauli ya viongozi wetu kuwa tupo tayari kwa vita ,kweli ni kauli nzito hasa ukizingatia kuwa vita haina macho ,hivyo viongozi wetu wanavyotoa kauli kama hizo binafsi naogopa sana kwani leo wanatuambia tupo tayari kwa vita ni lini tumefanya maandalizi ya kujiweka sawa kwa ajili ya vita?
Nawaomba viongozi wetu kujaribu kutafakari kwa kina kabla ya kutoa matamko mazito kama haya kwani hatujui hao Malawi wamepata wapi jeuri ya kutaka kutuchokoza na ikumbukwe Rais wao wa Malawi ni moongoni mwa viongozi walioukubari ushoga sasa isije ikawa ni mpango wa nchi marafiki na ushoga kutaka kutupiga kwa ajali ya viongozi wetu kutoukubali ushoga.
Ikumbukwe kuwa mipaka ambayo leo wanaitaka iliwekwa na wakoloni na siku zote hakukuwa na maneno leo wanadai kuwa hata jina la ziwa Nyasa limepewa ki makosa ilipaswa liitwe ziwa Malawi .
Nawaomba viongozi wetu kuomba kukaa chini na Malawi ili ikiwezekano basi tutafute jina moja ambalo litatumika katika ziwa hilo hata Likaitwa Nyasa -Malawi ama vinginevyo kwani vita si nzuri
Mungu ibariki Afrika ,Mungu ibariki Tanzania
0 comments:
Post a Comment