Na Amon Mtega, Iringa
MTU mmoja anayedhaniwa kuwa jambazi mkazi wa Mbinga mkoani Ruvuma akiwa na mwenzake, ameuawa na wananchi wakati wakitaka kumnyang’anya Sh milioni tatu mfanyabiashara Kayenga Paul wa Ipogoro wilayani Iringa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda, alisema tukio hilo lilitokea maeneo ya Ipogoro, Iringa.
Alimtaja mtu aliyeuawa kwa tuhuma za ujambazi kuwa ni Michael Mhonyo, ambaye baada ya kupekuliwa alikutwa na kitambulisho cha kupigia kura kinachomtambulisha kuwa ni Mkazi wa Mbinga mkoani Ruvuma.
Kamanda alisema katika tukio hilo, Kavenga Paul na mkewe, Rehema Kavenga wakiwa katika maeneo ya Ipogoro baada ya kufunga duka walivamiwa na majambazi wawili, mmoja akiwa na bastola.
“Katika tukio hilo majambazi hao walifyatua risasi nne hewani na kati ya hizo, moja ilimjeruhi Rehema kwenye kisigino cha mguu wa kulia na amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa na afya yake inaendelea vizuri,” alisema Kamanda huyo.
Baada ya wananchi kusikia milio ya risasi walitoka na kuwazingira majambazi hao na kumuua mmoja na mwingine mwenye bastola alikimbia na uchunguzi wa polisi naendelea.
Kamanda alitoa wito kwa wananchi kutotembea na fedha na badala yake kuziweka benki na wawe waangalifu wanapotembea na fedh nyingi kuomba ulinzi wa Jeshi la Polisi na Taasisi za Ulinzi.

Chanzo: Mtanzania
0 comments:
Post a Comment