MAKAMPUNI makubwa ya chai wilayani Mufindi yadaiwa kuwanyanyasa Wakulima wadogo wadogo wa zao la Chai kwa kuwacheleweshea fedha za malipo ya chai yao wanayoiuza katikka makampuni hayo.
kutokana na manyanyaso hayo wakulima hao wadogo wa chai wilayani wameiomba serikali na nchi wafadhili zilizopo kakika jumuiya ya Umoja wa ulaya kuwajengea viwanda vitakavyowawezesha kuuza majani makavu ya chai ili waweze kunufaika katika Soko la majani hayo na kumtoa mkulima katika umaskini.
mwenyekiti wa Chama cha wakulima wadogo wa chai Mkonge (Mkonge tea block farm ) , Santino Mdete alitoa Madai hayo mbele ya balozi wa Umoja wa ulaya, Filiberto Sebredondi alipowatembelea wakulima hao
Mdete alisema wakulima wa chai wameongezeka na uoteshaji wa miche ya chai katika vitaru vimeongezeka baada ya kujua umuhimu wake lakini wanashindwa kuhimili gharama za mbolea aina ya NPK 25-5-5-5 hivyo wanaiomba serikali kuweza kutoa rudhuku ya mbolea kwa wakulima wadogo wa chai kama ilivyo kwa zao la Mahindi na ngano.
Alisema heka moja ya shamba la chai inahitaji mifuko 12 ya mbolea ambapo mfuko mmoja unagharimu zaidi ya Sh 60,000 gharama ambayo mkulima mdogo hawezi kuimudu kutokana na kutokuwa na kipato cha kununua mbolea hivyo wanaiomba serikali kutoa rudhuku Kwao.
Mdete aliendelea kusisitiza kuwa wakulima wadogo huishia kuuza majani mabichi kwa wakulima wakubwa wenye viwanda/makampuni ya chai lakini wakiwa na viwanda vyao wataweza kuuza zaidi majani makavu ili kumuwezesha mkulima mdogo kuweza kunufaika kupitia kilimo cha chai.
Mdete alisema wakulima wakubwa wanawabana sana wakulima wadogo wa chai katika kununua majani mabichi lakini wakipata viwanda vyao watakuwa na wifi mpana wa kuuza majani makavu ya chai tofauti na sasa wanaishia kuuza majani mabichi ya chai.
Alisema kuwa zao la chai linazidi kukua katika wilaya ya Mufindi hivyo wakijengewa kiwanda chao wataweza kuwa na wigo mpana wa kujitanua kimaisha.
mtafiti wa maji na mimea wa taasisi ya utafiti wa chai Tanzania, Benjamini Mlaki alisema tafiti mbalimbali zilizofanyika imegundulika kuwa maji yanayotakiwa kutumika katika mashamba ya chai kwa wakulima wadogo wa chai ni asilimia 50 ya upungufu wa maji katika udongo.
Alisema kuwa wamekuwa wakifanya utafiti katika mashamba ya Kibena,Njombe na kufungua kuwa kiasi cha maji kinachotakiwa kutumika ni asilimia 50 ya upungufu wa maji katika udongo wa eneo la shamba na kuwa kwa sasa utafiti unaonyesha kiasi cha maji kinachohitajika kwa wakulima wadogo wa mashamba ya chai mkoani Tanga na Mbeya jambo ambalo litasaidia kukuza zao hilo na kumnufaisha mkulima mdogo mdogo.
Hata hivyo mkurugenzi wa utafiti chuo cha utafiti wa chai Tanzania, Dk Emmanuel Simbua alisema Tanzania ndiyo nchi inayoongoza duniani kwa kuwa na eneo kubwa la umwagiliaji wa chai ambapo hekta zaidi ya 5,000 zinapatikana nchini lakini sekta ya chai nchini inquires na nusu ya wakulima wadogo hivyo ubaguzi salaried mafunzo yatakayowanufaisha katika kilimo cha chai.
Dk Simbua alisema kwa kuwa serikali imeshaingia mikataba na kampuni ya vifaa vya kuendeleza umwagiliaji wa matone katika mashamba ya chai hivyonjuhudi zinafanyika ili kiwanda cha kutengeneza mashine za umwagiliaji wa matone watawajengea mazingira mazuri wakulima wadogo wa chai ili waweze kununua mashine hizo kwa bei nafuu.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment