Home » » SIKU MOJA BAADA YA KUPOKELEWA KAMA MFALME ,KANISA LA ASKOFU KAKOBE LAMFANYIA MAOMBI MBUNGE FILIKUNJOMBE

SIKU MOJA BAADA YA KUPOKELEWA KAMA MFALME ,KANISA LA ASKOFU KAKOBE LAMFANYIA MAOMBI MBUNGE FILIKUNJOMBE


SIKU
moja baada ya mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kupokelewa
jimboni na wapiga kura wake kama mfalme Kanisa la Full Gospel Bible
Fellowship(F.G.B.F) linaloongoza na askofu Zacharia Kakobe wilayani
Ludewa lamfanyia maombi maalum .


Huku mwenyewe akiahidi
kuendelea kupambana na Vitendo vya ufisadi kwa Taifa bila kuogopa na
kuwaomba Waumini wa Kanisa hilo na madhehebu mengine pamoja na wapiga
kura wake wote kuzidi kumwombea zaidi Kwani kazi iliyopo mbele yake ya
kupambana na ufisadi ni nzito yahitaji maombi.


Kanisa hilo
limfanyia mbunge Filikunjombe maombi hayo jana katika ibada maalum
ambayo iliandaliwa na uongozi wa Kanisa hilo kama njia ya kuungana na
vyama vya siasa na wananchi wa jimbo hilo kuutambua mchango na
kazi nzito ya mbunge huyo katika kupambana na vitendo vya ufisadi
nchini.


Katika maombi idaba hiyo Mchungaji wa Kanisa hilo Faustin Sambilanda.
alisema
kuwa kazi ilinayofanywa na Filikunjombe katika kulipigania Taifa
ni kubwa na hivyo kila mtanzania na kila kiongozi wa dini wanaowajibu
wa kuendelea kumwombea mbunge huyo na wengine ambao wapo kwa maslahi
ya watanzania .

Alisema kuwa uamuzi wa mbunge Filikunjombe
kuwemo katika orodha ya wabunge wasio na imani na waziri mkuu Mizengo
Pinda na kupelekea Rais Jakaya Kikwete kubadili baraza baraza
lake na mawaziri na kuwaondoa wale waliotuhumiwa kwa ufisadi si jambo
dongo na kuwa wananchi wa Ludewa wanaungana na watanzania katika
kuunga mkono uamuzi wa wabunge wapambanaji wa ufisadi akiwemo
Filikunjombe.

Hata hivyo alisema wanaweka utaratibu wa
kuendelea kumfanyia maombi maalum kwa ajili ya kazi nzito anayoifanya
ambayo silaha pekee ni maombi na si vinginevyo .

Kwa upande
wake mbunge Filikunjombe mbali ya kuupongeza uongozi wa kanisa
hilo la )F.G.B.F) kwa kuutambua mchango wake katika Taifa bado
alisema kuwa anatambua kazi nzuri inayofanywa na viongozi wa dini
katika jimbo hilo na kuwa yeye ni kiongozi wa makanisa na misikiti
yote katika jimbo hilo.

Alisema yeye ni mbunge wa wote na
wakati wote atawatumikia bila kuwabagua hivyo wakati wote ataendelea
kuwakutanisha Waumini na wananchi wote bila kuwabagua .

Mbunge
Filikunjombe alisema kuwa matumaini yake ni kuona yeye na wananchi wake
wataendelea kushirikiana na kuwa yeye alitakiwa kuwa Paroko kutokana
na awali kujikita zaidi kusomea uparoko ila sasa amekuwa mwanasiasa.

Japo
alisema kuwa kazi zote ni za kijamii na kuwa siku zote amekuwa
akiwaombea wanananchi wake wa Ludewa na kuwa lazima na wao wazidi
kumwombea ili kuendelea kuifanya kazi hiyo kwa kuongozwa na Mungu.

Hata
hivyo alisema kuwa alipaswa kufanya ziara katika maeneo mbali mbali ya
jimbo hilo ila kutokana na kikao cha bunge lijalo ni kwa ajili ya
bajeti hivyo hataweza kukosa na kuwaomba wapiga kura wake kuendelea
kumwombea ili aweze kuwawakilisha vema bungeni.bofya hapa

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa