Home » » Diwani Wa CCM Apandishwa Mahakamani Kwa Kutishia Kumuua Mbunge wa iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa na Diwani Wa Chadema Kata ya Mivinjeni

Diwani Wa CCM Apandishwa Mahakamani Kwa Kutishia Kumuua Mbunge wa iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa na Diwani Wa Chadema Kata ya Mivinjeni

 Mbunge wa Iringa(Chadema)Mch Peter Msigwa Akiongea na wafuasi wa chadema baada ya kesi kuhairishwa mpaka tarehe 30/5/2012 itakapotajwa tena
 Mbunge wa iringa Mjini Mch Peter Msigwa(Chadema) akifuatilia Kesi ndani chumba cha mahakama ya mkoa Iringa
 Mtuhumiwa
Wa kutishia Mauaji Diwani wa CCM kata ya Nduli Idd Chonanga akiwasili
mahakamani tayari kwa kusomewa mashitaka yanayomkabili
Wananchi Wakisubiri Kusikiliza Kesi Mahakamani Mapema leo.Picha zote na Said Ng'amilo-Iringa
---
Kutoka mahakamani
 Hakimu
mkazi wa mahakama ya mkoa wa iringa Bi Consolata Singano akiendesha
kesi huku akiongozwa na msoma mashtaka wa serikari Ndg msuya, alisema
kuwa Mshatakiwa anashitakiwa kwa makosa mawili, moja likiwa ni mnamo
tarehe 14/5/2012 katika ofisi za manispaa ya iringa alimtishia kwa
maneno Kumuua Mbunge wa Iringa mjini mch Peter Msigwa, shitaka la Pili,
tarehe hiyo hiyo alimtishia kumuua diwani wa kata ya
mivinjeni(Chadema)
Ndg Fredrick Nyalusi, Mshitakiwa alikana shitaka, hakimu alisema
dhamana ipo wazi kwa mshitakiwa, lakini wadhamini wa mshitakiwa
hawakutimiza masharti ya dhamana hivyo amepelekwa rumande.





Mbunge Msigwa naye asema haya

Mbunge
wa iringa Mch Peter msigwa amewataka wananchi  wa iringa kuwulivu
watulivu katika kipindi cha vurugu za kisiasa, wasiwe chanzo cha  fujo
na machafuko ya aina yoyote na waendelee na shughuli za ujenzi wa taifa
kama kawaida, ingawa ameshangaa mpaka sasa hakuna kiongozi wa serikari
ya mkoa aliyekemea kitendo hicho kisichokuwa cha kiungwana.

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa